Diwani kutoka Kata ya Hunyari iliyopo Halmashauri ya Bunda mkoani Mara Makina Josephat ametangaza kuhama Chadema na kuhamia CCM.
Makina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Bunda na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hiko kikuu cha upinzani ametangaza uamuzi huo leo jijini Dodoma na kupokelewa na MNEC wa CCM, Ismail Jamaa.
Akizungumza baada ya kumpokea Diwani huyo, MNEC Jamaa amesema wamempokea kiongozi huyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa na kwamba taratibu zingine za kumpokea zitafanyika wilayani Bunda ambapo anaishi.
Nae Makina amesema kwa miaka minne ambayo Rais Dk John Magufuli ameongoza amegusa kila sekta na kumaliza ajenda zote ambazo wapinzani walikua wakizipigania hivyo haoni haja tena ya kuendelea kuwepo upinzani.
Post a Comment