Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam Kisare Makori akizungumza wakati akifungua hafla ya kikao cha kazi cha Viongozi, Wafanyakazi na Wadau wa Maendeleo, iliyoandaliwa na Hashauri ya Manispaa ya Ubungo na kufanyika katika ukumbi wa Dariot Mbezi Magari Saba, Dar es Salaam, jana.
Baada Mkuu huyo wa Wilaya, kukamilisha ufunguzi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Beatrice Domini alitoa tathmini ya bajeti ya 2020/2021 kisha akawakaribisha Wakuu wa Idara zote za Halmashauri hiyo kutoa taarifa za kazi za Idara zao na baaye yalifuatia majadiliano kwa makundi mbalimbali yaliyokuwa ukumbini na kisha kutolewa majibu papo hapo kwa hoja zilizotolewa huku zile ambazo hazikuwa za kupatiwa majibu papo hapo zilizchukuliwa na uongozi kwa ajili ya kufanyiwa kazi. Kuona taswira kamili kupitia picha kem-kem za hafla hiyo? Tafadahali> BOFYA HAPA
Post a Comment