NA ELISA SHUNDA,MONDULI.
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Arusha, Mwishoni Mwa Wiki, Imemkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya Hiyo Taifa Ambaye Pia Ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Hicho, Dk.Edmund Mndolwa, Shilingi Milioni Moja kwa Ajili ya Kumchukulia Fomu ya Kugombea Nafasi ya Urais kwa Awamu ya Pili.
Akizungumza wakati akimkabidhi Mwenyekiti huyo fedha hizo Katibu mwenezi wa wilaya ya Arumeru ambaye pia ni mjumbe Wa kamati ya utekelezaji wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha Joshua Ongura alisema kuwa kutokana na tamko la Mwenyekiti wa jumuiya hiyo taifa alilolitoa December 2019 katika kongamano lililofanyika jijini Dar es salam wameona watoe fedha hizo
Alisema kuwa katika kongamano hilo jumuiya ya wazazi iliahidi kumchukulia fomu ya kugombea urais kwa awamu ya pili Mwenyekiti Wa chama hicho ambaye pia ni Rais Wa serikali ya awamu ya tano, Dk.John Pombe Joseph Magufuli.
Alisema kwa kuwa mkoa Wa Arusha unaanzia na alama A wameamua kuwa Wa kwanza kumchangia rais ,pia wameona watoe kwa kua raid ameweza kutekeleza vyema ilani ya chama ,na kutatua matatizo ya wananchi.
Akizungumza baada ya kuipokea Mwenyekiti Wa jumuiya ya Wazazi Taifa ambaye pia ni mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Edmund Mndolwa aliishukuru jumuiya hiyo kwa moyo walionyesha Wa kutoa fedha kwa ajili ya kumchukulia Rais fomu ya kugombea katika kipindi kingine.
Alisema aliahidi Rais kumchukulia fomu ya kugombea katika kipindi kingine ,ambapo alisema iwapo mikoa yote itatoa fedha hizo itapatikana jumla shilingi milioni 31 ambayo katika hizo watachukuwa shilingi milioni moja ya kumchukulia fomu Rais na fedha nyingine zitaingizwa kwenye kampeni yake.
Alizitaka mikoa mingine kuiga na kuanza kumchangia fedha ya fomu Rais kama vile mkoa Wa Arusha ulivyofanya na ulivyoanza kutoa fedha hizo mapema.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ambaye Ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Hicho, Dk.Edmund Mndolwa, Akipokea Fedha Tsh.Milioni Moja Kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya Hiyo Mkoa wa Arusha, Hezron Mbise (Kulia) kwa Ajili ya Kumchukulia Fomu ya Urais kwa Awamu ya Pili, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais, Dk.John Pombe Joseph Magufuli, Baada ya Kumaliza Kufungua Baraza la Mkoa Huo Lililofanyika Wilayani Monduli, Mwishoni Mwa Wiki. Katikati Ni Katibu Mkuu wa Jumuiya Hiyo, Mwalimu, Erasto Sima. Picha na Elisa Shunda.
Post a Comment