Featured

    Featured Posts

KAMATI KUU YA CCM YAIPA SIKU SABA KAMATI NDOGO YA UDHIBITI NA NIDHAMU KUKAMILISHA NA KUWASILISHA KWENYE VIKAO HUSIKA TAARIFA ZA KINA KINANA, MAKAMBA NA MEMBE

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya Itikadi na Uenezi  Humphrey Polepole,  akieleza yaliyojiri kwenye Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi, kilichofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Polepole alitoa maelezo hayo wakati wa Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally na Waandishi wa habari.







Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa siku saba kwa Kamati yake ndogo ya udhibiti na nidhamu kukamilisha na kuiwasilisha kwenye vikao husika, taarifa inayowahusu wanachama wake watatu, Makatibu Wakuu wawili wastaafu Mzee Yusuf Makamba na Kanali Mstaafu Abdulrahmani Kinana  na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe  ambao wote  wameshafika mbele ya Kamati hiyo.

Muda huo umetolewa na Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM katika kikao chake kilichofanyika leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema Kamati Kuu imefikia hatua hiyo, baada ya kupokea Taarifa ya awali kutoka kwa Kamati ya Usalama na Maadili juu ya utekelezaji wa azimio la Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) katika Kikao chake cha Mwezi Disemba 2019  kilichofanyika Jijini Mwanza.

Katika kikao hicho cha Jijini mwanza Kikao hicho kiliazimia kuwaita na kuwahoji wanachama watatu,  Yusuph Makamba, Abdulrahman Kinana na Benard Membe ambao Polepole amesema tayari wote wameshafika mbele ya Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu inayoongozwa na Mzee Philip Mangula, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.

Polepole amesema, Kamati Kuu  ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM pia imepokea taarifa ya Maombi ya Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ya kujiunga na CCM na kwamba Kikao hicho kimeridhia na kumpongeza Sumaye kwa uamuzi wake na kimeelekeza utaratibu wa kujiunga rasmi katika Chama ufuatwe kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Polepole amesema, Taarifa nyingine  kati ya tatu zilizowasilishwa kwenye Kikao hicho cha kamati Kuu ni ya Maendeleo ya Uandishi wa Waraka wa Kisera na kujiridhisha na kazi ambayo imekwisha kufanyika mpaka ngazi ya Rasimu.

"Kamati Kuu pia imepitia zoezi la uandishi wa Ilani ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na kuagiza maoni ya wadau mbalimbali kujumuishwa na kuzingatia ratiba ya kukamilisha uandishi wake ili vikao vya Chama vifanye uamuzi na kupitisha", alisema Polepole katika Mkutano wa waandishi wa habari na Katibu Mkuu was CCM, Dk. Bashiru Ally.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana