Kitabu cha MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY kilichotungwa na Mwanahabari Nguli nchini, Derek Murusuri na kuzinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda tayari kimeanza kupatikana katika maduka ya kuuza vitabu la TPH BOOKSHOP Dar es Salaam na VICTORY BOOKSHOP jijini Dodoma.
Kitabu hiki kinaelezea Waafrika kufikiri na kutekeleza mageuzi endelevu yatakayoifanya Afrika kuwa ni Bara lenye nguvu kubwa ya kiuchumi.
Kwa mujibu wa mtunzi wa kitabu hicho Bw. Derek Murusuri, kabla ya kuandika kitabu hicho alifanya utafiti kwa takriban miaka 21 na kwamba maudhui yaliyomo ndani ya kitabu hicho yataleta mabadiliko katika Afrika ijayo.
Post a Comment