Kamisheni ya Afya ya Kitaifa nchini China amesema kuwa, zaidi ya madaktari na manesi 1700 wameathirika na virusi vya Corona nchini humo.
Taaifa iliyotolewa na kamisheni hiyo jana Ijumaa mjini Beijing imebaini kuwa zaidi ya watu 1,500 kati ya madaktari na manesi hao, wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Hubei ambapo 1,102 miongoni mwao waliambukizwa virusi hivyo katika mji wa Wuhan, makao makuu ya mkoa huo. Taarifa hiyo hiyo imeongeza kuwa idadi ya maafisa hao wa afya walioambukizwa virusi hivyo inalingana na asilimia 308 ya waathirika wote wa maradhi hayo.
Kamisheni ya Afya ya Kitaifa nchini China imeendelea kufafanua kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha kwa maradhi hayo hadi kufikia Ijumaa ya jana ilikuwa ni 1468. Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi akizungumza na vyombo vya habari kando ya mkutano wa usalama mjini Berlin, Ujerumani amesema kuwa uchumi wa China utafufuka kwa nguvu kubwa na kwamba virusi vya Corona vitasambaratishwa.
Post a Comment