Featured

    Featured Posts

MAELFU YA WAMAREKANI WAANDAMANA

Washiriki katika maandamano hayo wamepiga nara za kupinga hatua hiyo ya Baraza la Seneti kama vile 'hatukubali kufichwa ukweli"' na 'tutakuondoa madarakani kwa kura zenu.'
Kwa mujibu wa duru za habari nchini Marekani, kwa akali miji 300 ya nchi hiyo imeshuhudia maandamano kama hayo ambapo mjini New York washiriki walipiga kambi mbele ya jesngo la Trump na kupiga nara za 'mtieni jela' na 'wewe ni mhalifu.' Vilevile polisi wamewatia mbaroni waandamanaji kadhaa ambao walipiga kambi ndani ya majengo ya Kongresi.
Maandamano dhidi ya Trump
Jeff Marcel, mjumbe wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni katika Bunge la Seneti ametuma video kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter inayomuonyesha akiwahutubia waandamanaji mbele ya jengo la Kongresi, na kuandika kuwa kile kilichoshuhudiwa katika Baraza la Seneti si kumalizika kesi inayomkabili Trump bali ni kufichwa ukweli na uhakika. Ameendelea kusema kwamba ushawishi wa rais umepenya hadi ndani ya Seneti na sasa nguvu za bunge hilo ni tishio kwa Wamarekani.
Kwsa upande wake Ayanna Pressley ambaye pia ameshiriki maandamano hayo ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba: 'Katika mfumo huu wa demokrasia ninyi (maseneta) mnawajibika mbele ya wananchi. Tutaendelea kuonyesha hasira zetu kwa ajili ya kutafuta haki na uadilifu.'
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana