Featured

    Featured Posts

MAGWIJI WA MICHEZO WALIOWEKA HISTORIA YA KIPEKEE NCHINI TANZANIA



Pichani Ni Jenerali Mirisho Hagai Sarakikya (Kati) Akiwa Na Wanariadha Mabingwa Wa Dunia Wa Zamani, Filbert Bayi (Kushoto) Na Juma Ikangaa.  Hawa Ni Watu Watatu Ambao Mjina Yao Yanastahili Kuandikwa Kwa Wino Wa Dhahabu Katika Vitabu Vya Kumbukumbu  Ya Historia Ya Riadha Na Michezo Nchini Tanzania. Hilo Halina Ubishi...

Tukianza Na Jenerali Sarakikya, Yeye Ndiye Alikuwa Mkuu Wa Majeshi Wa Kwanza Mara Tu Bada Ya Tanganyika Kupata Uhuru Mwaka 1964 Na Akatumikia Wadhifa Huo Kwa Miaka Kumi Yaani Toka Hiyo 1964 Hadi Alipostaafu Mwaka 1974. 
Wakati Anapata Cheo Kuwa CDF Jenerali Sarakiya Pia Alikuwa Ndiye Mwenyekiti Wa Chama Cha Riadha Cha Tanzania (TAA) Kuanzia Mwaka 1962 Hadi Mwaka 1972.
Ikiwa Hiyo Haitoshi Mara Baada Ya Kustaafu Jeshini Mwaka Huo Huo Wa 1974, Mwalimu Nyerere Alimteua Jenerali  Sarakikya Kuwa Waziri Wa Michezo, Vijana Na Utamaduni.
Ukiangalia Katikati Ya Mistari Utamaizi Kwamba Historia Ya Mafanikio Ya Riadha Na Michezo Kwa Ujumla Nchini Tanzania Yalikuwa Katika Miaka Hiyo Ambayo Jenerali Sarakikya Alikuwa Mwenyekiti Wa TAA, Mkuu Wa Majeshi Na Baadaye Waziri Wa Michezo, Vijana Na Utamaduni.
Huo Ndio Wakati Wanariadha Filbert Bayi, Juma Ikangaa, Suleiman Nyambui, Gidamis Shaganga, Mwinga Mwanjala, Nzaeli Kyomo Na Wengi Wengine Walikuwa Wanang’ara Kwenye Medani Za Kimataifa.
Kwa Hiyo Picha Hii Ni Kubwa Na Yenye Historia Nzito Kwa Kadri Mafanikio Katika Michezo Kwa Nchi Hii Yanahusika.
Wote Watatu Ni Wanajeshi Wastaafu, Kwani Filbert Bayi  Baada Ya Ushindi Wake Alipandishwa Cheo Hadi Kuwa Luteni, Na Baada Ya Kuhudhuria Mafunzo Ya Afisa Kadet Huko Monduli Mwaka 1977 Alipanda Kuwa Kepteni. Hadi Anastaafu Mwaka 2001 Alikuwa Na Cheo Cha Meja Kitengo Cha Ufundi Wa Ndege Jeshini.
Kwa Upande Wa Ikangaa, Yeye Alikuwa Mkurugenzi Wa Michezo Makao Makuu Ya Jeshi Hadi Alipostaafu Kwa Mujibu Wa Sheria Akiwa Na Cheo Cha Kanali. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana