Featured

    Featured Posts

MAKATIBU WAKUU WASTAAFU WA CCM MZEE MAKAMBA NA KINANA WAITIKIA WITO WA KAMATI NDOGO YA USALAMA NA MAADILI, LEO


 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Abdulrahaman Kinana akiwa ofisini kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula baada ya kuitikia wito wa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili ya CCM, leo.

 
 
Katibu Mkuu mstaafu wa CCMJ, Yusuf Makamba akiagwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Dk. Bashiru Ally baada ya kuitikia wito wa Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili ya CCM.



Makatibu Wakuu Wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuf Makamba na  Abdulrahaman Kinana leo Februari 10, 2020 wamefika katika Ofisi Ndogo za CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam kuitikia wito wa Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili inayoongozwa na Philip Mangula.

Makatibu Wakuu hao Abdulrahman Kinana na Ndg. Yusuf Makamba wamefika katika Ofisi hizo majira ya mchana na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally Kakurwa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana