Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Beatrice Dominic na Meneja Mkuu wa Lancet Laboratories Tanzania Nassoro Salim wakitia saini mkataba wa ushirikiano kati ya Manispaa na Kampuni hiyo ili kutanua maabara na kuongeza aina na idadi ya vipimo vitakavyokuwa vikifanyika katika hospitali ya Sinza iliyopo katika Manispaa hiyo, jana, KWA PICHA ZAIDI ZA UTIAJI SAINI MKATABA HIYO>>BOFYA HAPA
SINZA, Dar es Salaam
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imesaini Mkataba wa ushirikiano na kampuni ya Lancet Laboratories kwa lengo la kutanua maabara na kuongeza aina na idadi ya vipimo vitakavyokuwa vikifanyika katika hospitali ya Sinza iliyopo katika Manispaa hiyo.
Utiaji saini huo ulimefanywa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic na Meneja Mkuu wa Lancet Laboratories Tanzania Nassoro Salim katika Hospitali ya Sinza Palestina ukishuhudiwa na Mganga Mkuu wa Manispaa Dk. Peter Nsanya, Mwanasheria wa Manispaa Kissa Mbilla, baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo na baadhi ya wafanyakazi wa Lancet.
Mganga Mkuu wa Manispaa Dk. Peter Nsanya alisema kwamba Manispaa imesaini mkataba huo sio tu kwa manufaa ya wananchi wanaoishi Ubungo bali kwa wananchi wote wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
”Niseme tu kwamba vipimo vitakavyokuwa vinafanyika hapa si chini ya vipimo mia tatu ikiwemo cancer na homa ya ini” alisema Mganga Mkuu.
Nae Meneja wa Lancet Tanzania Nassoro Salim, alisema kuwa jana ilikuwa ni siku ya furaha sana kwake kwa kufanikisha Lancet kufanya kazi na Ubungo nia ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya upande wa vipimo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic alimshukuru Meneja wa Lancet Tanzania kwa kukubali kusaini mkataba huo na kusema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuboresha huduma kwa wananchi hasa kwenye sekta ya Afya na ndicho anachokifanya.
”Nawaahidi Lancet kuwa tutatoa ushirikiano wa kutosha, na natoa rai kwa watumishi wote kushirikiana vizuri na Lancet. Tayari tumeshafanya mazungumzo na Benki ya NMB ili wawepo hapa na malipo yote yawe yanafanyika benki”. Alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema baada ya mwezi mmoja hospitali ya Sinza itaanza kupokea wagonjwa ambao walikuwa hawafiki hospitalini hapo kwa hofu ya kutokuwepo baadhi ya vipimo na sio tu kwamba itaboresha huduma bali pia itasaidia kuongeza mapato.
/IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
MANISPAA YA UBUNGO
Post a Comment