Meli moja ya kitalii ambayo ilikuwa imekwama isijue pa kwenda baharini, kutokana na wasiwasi wa bandari kuhusu uwezekano wa kubeba abiria walioambukizwa virusi vya corona hatimaye imetia nanga nchini Cambodia.
Lakini Westerdam ilio na zaidi ya abiria 2000 pamoja na wafanyakazi haina maambukizi yoyote. Siku ya Jumanne , meli hiyo ilijaribu kutia nanga nchini Bangkok lakini ikanyimwa ruhusa.
Meli ya wanamaji wa Thai iliisindikiza hadi nje ya ghuba la Thailand ambapo ni kutoka hapo ilipoamua kuelekea Cambodia. Siku ya Alhamisi , meli hiyo hatimaye iliwasili katika eneo la kutia nanga katika mji wa bandari ya Sihanoukville.
''Mapema leo asubuhi , kuona ardhi ilikuwa kitu muhimu sana'' , alisema abiria Angela Jones kutoka Marekani akizungumza na Reuters, ''Nilidhani Je huu ni ukweli?''.
Meli hiyo ilikuwa imetarajiwa kuzunguka kwa wiki mbili na katika siku hizo 14 kulikuwa na matatizo ya kuisha kwa mafuta mbali na chakula.
Mbali na Thailand , pia ilifukuzwa na Taiwan, Guam na Japan.
''Tumekuwa na bahati mbaya chungu nzima, tulidhani tunaenda nyumbani kabla ya kufukuzwa'', alisema bi Jones .
Nahodha wa meli hiyo Vincent Smit alisema kwamba meli hiyo itatia nanga nje
Sihanoukville iliruhusu mamlaka kufanya ukaguzi wa kiafya ndani ya meli hiyo.
Post a Comment