Na Woinde Shizza Arusha
SERIKALI kupitia kwa mkurugenzi wa huduma za mifugo Tanzania Prof.
Herzon Nonga imetoa ufafanuzi wa kitaalamu juu ya Ng’ombe
aliezaliwa na midomo miwili pamoja na macho matatu na kubainisha
kuwa tukio hilo ni lakawaida kwani kutokea ambapo katika ndama elfu
2000 wanaozaliwa kunaweza kukawa na mnyama mwenye ulemavu wa viongo mmoja au kutokuwepo kabisa
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa huduma za mifugo Tanzania Prof.
Herzon Nonga wakati akiongea na gazeti hili jana ambapo alisema kuwa
mnyama anaweza kuzaliwa na ulemavu kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo ulemavu wa kurithi ,ambapo Yule ndama anarithi vinasaba
kutoka kwa wazazi wake ambao huu huchangia kwa asilimia 20 % na
ulemavu mwingini ni ule unaosababishwa visababishi vyenye sumu
ambao ulemavu huu huchangia kwa asilimi 90% kutokea kwa wanyama.
Alisema ulemavu unaotokea kwa wanyama hutokea kwa asilimia chache
sana kati ya asilimia 0.3% kwa wanyama wote wanaozaliwa ambapo
unaweza kuonekana kwa mifugo na mwingine hauwezi kuonekana kabisa kwa macho ambapo alisema kwa kwa upande wa mifugo huwa wanashauri
iwapo mnyama atazaliwa akiwa na ulemavu basi mnyama yule atenganishwe na wenzake na kama ni ndama aondolewe au aharibiwe (awawe kabisa ) ,na mama yake achinjwe kabisa kwani akiachwa anaweza akaendelea kuzaa ndama wengine wenye ulemavu na serikali haiitaji kufuga ng’ombe wenye ulemavu .
Alisema ulemavu wenye visababishi unatokana na mazingira ambayo
mnyama yupo ,ambapo huu unasababishwa na mambo mengi ikiwemo vyakula,kemikali ,maumivu ambapo kwa upande wa maumivu alifafanua kuwa iwapo Ng’ombe au mnyama akipigwa na kitu kizito katika tumbo vinaweza kuwa kisababishi , kingine ni mionzi mfano ya exray, sumu ambazo zinapatikana kwenye majani kwa mfano akila majani yale ambayo
yamepuliziwa viuatilifu pamoja na maambukizi hasa ya virusi.
“tukianza kuangalia visababishi vinavyotokana na mazingira moja wapo
inaweza ikawa ukosekana ji au upungufu wa vyakula mwilini ikiwemo
madini au mineral na mineral ni madini ambayo yapo kwenye vyakula
kama kopa ,upungufu wa madini haya unaweza kumpelekea mnyama au kiumbe Yule a anatengenezwa kule tumboni akatoka ajakamilika au mlemavu kama alietokea hapo Arusha, kwenye vyakula pia kunaweza kuwa mnyama anaupungufu wa vitamin mfano A au B na akitokea upungufu huu ndio unakuta mnyama anazaliwa labda anaweza kuwa na matege ,”Alibainisha Nonga.
Alisema upungufu mwinge ni wa kimazingira ambapo mnyama anaweza
akala vitu vibaya , vitu vibaya vipo katika makundi mawili yaani kemikali za mashambani za kuuwa wadudu za kuuwa magugu, zile zinazotumika viwandani na ng’ombe Yule mwenye mimba akala yale majani
yenye kemikali hizo kama hazikusababisha mimba ile kutoka basi
zitasababisha ndama anaejengeka kule kwenye tumbo la uzazi akizaliwa
kuwa na ulemavu .
Alizitaja kemikali zingine ambazo zinatokana na majani yenye sumu ni
pamoja na majani yenye jamii ya Tumbaku ,majani yenye jamii ya
kabeji ambapo ng’ombe akila majani haya akiwa na mimba yanaweza
kumsababishia mimba kutoka au kumsababishia kiumbe kutoka na ulemavu
,kundi lingine la usababisha ni pamoja na maambukizi ya maradhi
mbalimbali hususani ya yale ya virusi ambapo kwenye ngombe kuna
virusi mbalimbali ambapo virusi hivi vinaenda kukaa kwa ndama na
ndama atakae zaliwa anakuwa ameathirika moja kwa moja
“Pale ambapo ng’ombe anapigwa na kitu kizito tumboni akiwa na mimba ,
ambapo Yule ndama asipotoka kwa mimba kuharibika ,akikaa atatoka akiwa na ulemavu ,au mfuko wa mimba unaweza ukajikusanya ukajiviringisha na kumbana kiumbe Yule aliopo tumboni ikampeleka kuzaliwa akiwa mlemavu wakichwa au wingine huzaliwa hata miguu ukiwa
mifupi”alibainisha .
Aidha alisema Ulemavu mwingi unaotokea kwa mifugo ni ule ambao
unahusisha mifupa migumu ,mifupa milaini na Jointi ambapo alisema kwa
upande wa mnyama huyu wa midomo miwili na macho matatu ni kwamba
kulitokea muingiliano wa visababishi mbalimbali uliopelekea ndama
huyo kuzaliwa kama alivyozaliwa ,huku akifafanua kuwa ndama yule
alikuwa awazaliwi mapacha kama watu wanavyozani bali ni muingiliano
huo ndio umesababisha kuzaliwa hivyo na ulemavu huu .
Picha ikionyesha ngombe aliyezaliwa na midomo mitatu na macho matatu katika Kijiji cha ngiresi kata ya sokoni 2ndani ya halmashauri ya Arusha. Mkoani Arusha ,ngombe huyo alizaliwa February 2020 na hadi sasa anasiku 20 ngombe huyo amekuwa gumzo kwa wilaya hiyo.
Mmiliki wa ngombe, Hugo Eliakimu Mongasi akionyesha jinsi ndama Huyo alivyozaliwa ambapo alisema alipomuona mnyama Huyo alishituka sana ila yeye binafsi anaamini ni mipango ya mungu na sio ushirikina (picha na Woinde Shizza,Arusha).
Post a Comment