Featured

    Featured Posts

PINDA: AWATAKA WATANZANI KUACHA KASUMBA YA KUAMINI WAGENI KWENYE UWEKEZAJI

Na Baraka Messa, Songwe
WAZIRI Mkuu mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda amewataka watanzania kubadilika kwa kuacha Kasumba ya kuamini wageni kuja kuwekeza katika fulsa mbalimbali zilizopo nchini ili kufikia uchumi wa kati ambao utaboresha maisha ya watanzania kwa ujumla.

Pinda alikuwa mgeni rasmi katika kufunga Kongamano la biashara Mkoani Songwe  alitanabaisha kuwa ili kufikia uchumi wa kati ambao Rais Magufuli anausisitiza ifikapo 2025 alisema watanzania wanatakiwa kubadilika kwa kiasi kikubwa kwa kuwekeza kwenye fursa mbalimbali muhimu ambazo zitabadilisha maisha yao na Taifa kwa ujumla.

Alisema mkoa wa Songwe ni miongoni mwa mikoa ambayo inafursa nyingi za uwekezaji kutokana na kuwa ni lango la kuu la nchi 16 za kusini mwa afrika zilizopo kwenye Jumuiya ya SADC ambapo wenyeji wanatakiwa kuwa wawekezaji namba moja kabala ya kutoa kipaumbele kwa wageni.

Alizitaka Halmashauri zote kuacha urasimu pindi wawekezaji wa ndani wanapotaka kuwekeza badala yake aliwasisitiza kuandaa elimu ya kuwahamasisha na kuanda mazingira mazuri ya miundo mbinu iliyobora ili dhana ya uchumi wa kati iweze kutimia na kuwanufaisha wazawa.

“Lengo la kugawa mkoa wa Mbeya nikiwa madarakani na kuzaliwa mkoa wa Songwe ilikuwa ni kusogeza huduma karibu kwa wananchi na kusukuma maendeleo ambapo ikiwa ni pamoja na kuwa karibu na wawekezaji wa ndani ambao ndio wanakuza uchumi kwa kiasi kikubwa, tuhakikishe mwananchi wa Songwe ananufaika kwa kuanzishwa viwanda vitakavyo chukua malighafi kutoka kwa mkulima, mvuvi na mfugaji wa Songwe ili kukomesha adui umasikini,

Adui mkubwa kwenye uwekezaji wa ndani kwa nchi yetu ni urasimu unaturudisha sana nyuma Rais wa awamu hii ya tano anapigana sana kuhakikisha nchi inafikia kwenye uchumi wa kati, mtu anakuja kwa ajili ya kuwekeza kwenye ardhi lakin anazungushwa mpaka atoe rushwa , watu wa aina hii wanaokwamisha uwekezaji wachukuliwe hatuwa na kuwekwa ndani” alisema Pinda

Aliongeza kuwa fursa nyingi zilizopo Songwe kama kilimo, madini, viwanda na utalii zipo ndani ya uwezo wa wazawa  wa Songwe na watanzania kwa ujumla ambapo wakibadilika na kuwekeza kwanguvu kutabadilisha kwa kiasi kikubwa uchumi wao na nchi.

“Tukiwekeza sisi wazalendo tutanufaika zaidi kwa sababu watakaoajiliwa watakuwa ni watoto wetu tofauti na tukitoa kipaumbele kwa wenyeji tutaendelea kutonufaika na nchi yetu kwa sababu hata wafanyakazi kwenye viwanda watatoka nje ya nchi yetu” aliongeza Pinda.

Sanjali na hilo Pinda alisema kuwa kupitia Kongamano la Songwe lililokuwa na kauli mbiu ya ‘’Wekeza Songwe lango kuu la SADC” na kuzindua kitabu maalum kwa ajili ya kutangaza fursa za uwekezaji Songwe kumeutangaza mkoa huo katika ramani ya dunia na kuwataka viongozi wa Songwe kusambaza nakala ya kitabu katika balozi za nchi mbalmbali ili kuwavuta wawekezaji na watalii kuja Songwe baada ya kusoma kitabu hico.

Naye mwanasiasa mkongwe nchi Christian Mzindakaya alizitaka Taasis za kifedha kutoa mikopo nafuu kwa wawekezaji wadogo na wakulimawa Tanzania ili kuongeza uzalishaji ambao utapelekea viwanda kupata malighafi kwa wingi na kupelekea nchi kufiakia uchumi wa kati.

Alisema maegeuzi ya kweli kwa wawekezaji wadogo nchini ni Taasis hizo kubadilika kwa kutoa mikopo yenye unafuu kwao ili kuongeza uz

‘’Hakuna mkulima duniani ambaye ameendelea bila mikopo hizi benki zilizopo hazimsadii mkulima dawa ni kuanzisha benki ya kanada ya mkulima ambayo itajumuisha mikoa yote ya kanda ya kusini ili kumsaidia mkulima  wa Tanzania , Nchi kama Marekani imeendelea kimiundombinu na uchumi ni kwa sababu ya kumthamini kwa kiasi kikubwa mkulima na mwekezaji mdogo” alisema  Mzindakaya.

 Awali katibu tawala mkoa wa Songwe David Kafulila alisema kuwa Mkoa wa Songwe wamejipanga kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya ajila kwa kutengeneza ajira kwa wasomi wengi waliomaliza vyuo vikuu kwa kuwapa elimu ya kuwekeza kwenye ufugaji wa nyuki amabao ni uwekezaji ambao unafaida kubwa kutokana na soko la mazao yatokanayo na nyuki.

Alisema Songwe kuna misitu mingi ambayo inafaa kwa ufugaji wa nyuki , lakini pia mkoa umetenga zaidi ya hekta 6000 kwa ajili ya ufugaji wa nyuki ambayo watapelekwa wawekezaji mbalimbali katika maeneo hayo ili kuogeza uzalishaji na kutatua chanagamoto ya wasomi kufikria kuajiliwa pekee.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana