Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mapema leo Jumanne kwamba, RAIS Mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi, 1924 – 2020, amefariki.
Mzee Moi amefariki duniia katika Hospitali ya Nairobi ambako amekuwa akitibiwa mara kwa mara.
Rais Kenyatta ametangaza kuwa Mzee Moi, amefariki dunia leo asubuhi.
Msaidizi wa kibinafsi wa Mzee Moi, Lee Njiru pia amethibitisha kuwa Rais huyo wa pili wa Kenya ameaga dunia.
Rais Kenyatta anatarajiwa kutoa taarifa kamili baadaye kuhusu habari hiyo.
Mzee Moi amekuwa akilazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu mwaka 2019.
Moi alitawala Kenya kwa miaka 24 tangu 1978 hadi 2002.
Moi alikuwa rais wa Kenya kwa kipindi cha miaka 24 kabla ya kuacha madaraka mnamo 2002 baada ya Wakenya kumchagua kwa kura nyingi Mwai Kibaki aliyechukua nafasi ya Moi.
Daniel Arap Moi aliingia madarakani mwaka 1978 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta.
Post a Comment