Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akizungumza na viongozi wa mkoa huo.
Na Lydia Lugakila-: Kagera
Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameagiza viongozi wa ngazi zote mkoani Kagera kuacha Mara moja masuala ya migogoro na mivutano inayovuruga amani na kukwamisha maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.
Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ametoa agizo hilo katika kikao maalum cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo.
Brigedia Jenerali Gaguti amesema kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu ambapo kila mtu atanufaika endapo hali ya usalama ikiwepo na kuwa kuagiza viongozi wa ngazi zote kutojihusisha na masuala ya migogoro pamoja na mivutano inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mkuu huyo wa mkoa amesema viongozi wanatakiwa kufanya yaliyo mema kwa ajili ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuhimiza maendeleo na kuongeza kuwa kama kuna migogoro viongozi wahusishe watu kama viongozi wa mkoa ili kumaliza tofauti zao.
Brigedia Gaguti ameongeza kuwa huu sio muda wa migogoro badala yake kila kiongozi kwa nafasi yake ajitafakari na kupanga mipango ya maendeleo.
"Si vyema Januari hadi Desemba watu mnakaa na migogoro isiyokuwa na maana mnavutana vutana muda huo umeisha na kubakia muda wa kazi za maendeleo" alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Ameongeza kuwa tofauti za aina yoyote zinatakiwa kumalizika kupitia chama, serikali na Taasisi husika.
Hata hivyo viongozi ngazi zote kutimiza wajibu wao, kuweka nguvu kubwa katika kufanya maendeleo badala ya mivutano inayorudisha maendeleo nyuma.
Post a Comment