Featured

    Featured Posts

TUNAKABILIWA NA UHABA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA WHO

  Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus ameonya kuwa ulimwengu unakabiliwa na uhaba wa vifaa maalum vya kufunika uso pamoja na vifaa vingine vya kujikinga na virusi vya Corona. 

Akizungumza leo katika kikao cha bodi ya wakurugenzi wa WHO mjini Geneva, Ghebreyesus amesema mapema wiki hii walianza kupeleka vifaa hivyo kwenye nchi zinazohitaji msaada. 

Ghebreyesus amesema hadi sasa virusi vya Corona vimesababisha vifo vya watu 637 nchini China na wengine 31,211 wameambukizwa. 

Amesema katika siku mbili zilizopita pamekuwa na taarifa chache za watu walioambukizwa virusi hivyo nchini humo ambayo ni habari njema. 

Hata hivyo, ametahadharisha kuhusu kuzitegemea zaidi takwimu hizo, kwani idadi ya waathirika inaweza kuongezeka tena. 

Mkurugenzi huyo wa WHO, amesema kuna baadhi ya nchi zimeshindwa kutoa takwimu kamili za kitabibu za watu waliothibitika kuambukizwa virusi vya Corona.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana