Featured

    Featured Posts

UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA WAANZA DAR,PWANI

Na Richard Mwaikenda

WAKAZI wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi

la Uboreshaji wa Daftari Kudumu la Wapiga Kura ulioanza Februari 14 na kumalizika Februari 20 mwaka huu.

Mwito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu,Semistocles Kaijage wakati wa mkutano na Wadau wa Uchaguzi wa Mkoa wa Dar eSalaam hivi karibuni.

"Ninayo furaha sasa kuwafahamisha kuwa maandalizi kwa ajili ya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika kundi la mikoa ya Dar eS Salaam na Pwani yamekamilika,"alisema Jaji Kaijage na kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji huo.

Alisema hivi sasa Tume imekamilisha  zoezi la uboreshaji takribani mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani isipokuwa Dar es Salaam na Pwani, wanayomalizia wiki ijayo.Tanzania ina mikoa 31. Bara 26 na Visiwani mitano.

Uboreshaji wa safari hii hauhusishi Wapiga Kura wote walioandikishwa 2015, bali unawahusu

Wapiga Kura  wapya  ambao wametimiza umri wa miaka 18 na wale watakaotimiza umri wa miaka 18 siku ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Pia unahusisha waliohama kutoka  maeneo yao ya awali  kuhamia maeneo mengine, wenye kadi

zilizoharibika au kupotea na wanaotakiwa kuondolewa  kwenye Daftari kama vile waliofariki au kupoteza sifa.

Uboreshaji huu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unafanyika kwa kutumia  Teknolojia ya Kielektroniki ya Biometriki (BVR). Teknolojia hii huchukua taarifa ya mtu za kibailojia

na kuzihifadhi katika Kanzidata (Database) kwa ajili ya utambuzi na ndio iliyotumika kuandikisha Wapiga Kura mwaka 2015. 

Jaji Kaijage, aliwaomba Wadau wa Uchaguzi kusaidia kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kuhakiki taarifa zao wakati wa zoezi la uboreshaji litakaloendeshwa kwa siku saba katika mikoa hii iliyobakia.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana