Featured

    Featured Posts

VIONGOZI CCM KIBONDO WAHIMIZWA KUSIMAMIA ILANI YA CCM IPASWAVYO

Na Jastin Cosmas, Kibondo
Mwenyekiti wa Chamam Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kigoma Amantusi Nzamba amewataka viongozi wa CCM  Wilayani Kibondo kufanya kazi ipasavyo ili kuweza kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM vizuri.

Hayo ameyasema katika maadhimisho ya miaka 43 ya Chama Cha Mapinduzi yaliyofanyika jana katika Wilaya ya Kibondo ambapo Mwenyekiti huyo alipata fursa ya kutembelea baadhi ya shule za sekondari wilayani hapa ikiwemo shule ya Sekondari Maragarasi na kushiriki shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauli ya Kibondo Ndugu Rutema alisema idadi ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa darasa la saba na kujiunga na kidato cha kwanza inazidi kuongezeka hivyo wananchi hawana budi kuchangia nguvu kazi na serikali kumalizia pale walipo ishia.

Nae Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Kajoro Vyoholoka amesema CCM imekuwa na mafanikio makubwa hivyo wananchi hawana budi kuchagua kiongozi bora atakae tatua changamoto za wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana