Featured

    Featured Posts

WANAOSHINDWA KUKUMBUKA MAJINA YAO HUCHELEWESHA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA-JAJI KAIJAGE

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jaji Semistocles Kaijage akizungumza na mkutano na wadau wa uchaguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam wa kupeana taarifa juu ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani utakaoanza wiki ijayo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA



Na Richard Mwaikenda

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), amesema kitendo cha baadhi wananchi kushindwa kukumbuka majina yao, kinasababisha ucheleweshwaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura.

Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa Wadau wa Uchaguzi, jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alipokuwa akitaja baadhi ya changamoto zinazolikabili zoezi hilo.

"Wapiga Kura kushindwa kukumbuka majina yao  wanapokwenda  kituoni kwa ajili ya kurekebisha  taarifa zao na hivyo kuchukua  muda mrefu katafuta majina yao kwa usahihi," alisema Jaji mstaafu Kaijage.
Alitaja Changamoto nyingine kuwa ni kuwepo kwa idadi kubwa ya wananchi waliopoteza kadi zao za kupigia kura ama kadi zao  kuharibika.  Nitoe rai kwenu kuwakumbusha wapiga kura kuhakikisha wanatunza kadi zao hadi siku ya uchaguzi na hata baada ya hapo.

Katika maeneo mengi kumekuwepo na hali ya watu kujitokeza kwa wingi siku za mwishoni ili kuboresha taarifa zao au kujiandikisha  na hivyo kusababisha misururu mirefu kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura. Jambo hili linaweza kuepukika   kama wananchi watajitokeza mapema pindi zoezi linapoanza.


Jambo lingine ni wananchi wengi katika baadhi ya maeneo kushindwa kutofautisha Daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara. Tume kupitia Elimu ya Mpiga Kura inaendelea na juhudi za kutoa ufafanuzi juu ya utofauti wa Chaguzi hizi na mamlaka  zake za Usimamizi.

Changamoto nyingine ni zoezi hili kufanyika katika kipindi cha mvua kwenye  baadhi ya maeneo na hivyo kuathiriwa na miundombinu ya  barabara. Hata hivyo, Tume ilijipanga kukabiliana na hali hiyo,  na kuweza kufikisha vifaa kwa wakati bila kuathiri ratiba ya kufanyika kwa uboreshaji. Kwa  upande wa vituo vya kujiandikisha vilivyo katika maeneo ya wazi Tume iliandaa mahema.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana