Featured

    Featured Posts

YATANGAZA JANGA LA TAIFA

Wizara ya Kilimo ya Somalia ilisema jana (Jumapili) kwamba wimbi kubwa la nzige waliovamia maeneo ya jangwani ni hatari kubwa kwa nchi hiyo ambayo tayari ina mazingira mabaya ya usalama wa chakula.
Taarifa ya wizara hiyo imeongeza kuwa, chakula cha wanadamu na mifugo yao kiko hatarini Somalia. Wimbi la nzige walioivamia nchi hiyo ni kubwa na wanaangamiza kiwango kikubwa cha mazao, mimea na majani.
Wizara hiyo imesema, tahadhari ya taifa iliyotangazwa na wizara hiyo inalenga kuhamasisha juhudi zaidi za kupambana na janga hilo na kushajiisha mataifa kuisaidia Somalia kwani kuvamiwa na nzige wakati huu wa kabla ya mwezi Aprili ambacho ni kipindi cha mavuno ni jambo hatari sana.
Nzige ni jamii ya panzi na wanapovamia shamba huangamiza kila kitu na kusababisha kutokea janga la njaa. 
Mbali na janga la nzige, Somalia inakabiliwa pia na ukame na usalama mdogo wa chakula

Waziri wa Kilimo wa Somalia, Said Hussein Iid amesema kuwa, kama hatua hazitachukuliwa hivi sasa, basi nchi hiyo itakumbwa na upungufu mkubwa wa chakula ambao itashindwa kukabiliana nao. Amesema, wametoa tahadhari hiyo kama njia ya kulinda usalama wa chakula kwa wananchi wa Somalia.
Kwa muijibu wa Kundi la Usalama wa Chakula na Lishe (FCNWG), eneo la Afrika Mashariki tayari lina usalama mdogo wa chakula huku watu milioni 19 wa eneo hilo wakikabiliwa na janga kubwa la njaa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana