|
Imeelezwa kuwa zaidi ya kiasi cha shilingi Bilioni 25 zitatumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara zilizoathiriwa na mvua nyingi zilizonyesha toka kipindi cha mwisho wa mwaka 2019.
Amezungumza hayo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati akiwa mkoani Shinyanga akiendelea na ziara yake ya kukagua athari za mvua katika miundombinu ya barabara.
Naibu Waziri Kwandikwa amekagua barabara inayotoka Kahama kuelekea Mwananga yenye urefu wa kilometa 148 ambapo sehemu ya barabara hiyo imeathiriwa na maji mengi yanayopita kwenye mkondo wa Ziwa Victoria.
"Hii ni barabara fupi inayounganisha wakazi wa Kahama na Mwanza kupitia Solwa ambapo kilometa 2. 3 ndizo zilizoathirika na hivyo kufanya mawasiliano ya wananchi hawa kuwa ni ya kuzunguka na muda kuongezeka", amesema Naibu Waziri huyo.
Ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo tayari usanifu wa kina ushafanyika na hivyo Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami.
"Mvua hizi pia zinatupa sisi fursa ya kutazama eneo hili upya kwa kuhakikisha usanifu wetu unaenda sambamba na hali iliyojitokeza na hii itangaliwa maeneo yote nchini", amefafanua Naibu Waziri Kwandikwa.
Ametoa wito kwa wasafirishaji wanaotumia barabara hiyo kutowasumbua wananchi kwa kutumia barabara hiyo na badala yake watumie barabara ya lami ile itokayo Kahama - Isaka - Tinde mpaka Mwanza kwa kuwa inapitika vizuri kabisa.
Aidha, ameeleza mkakati wa Serikali katika kipindi hiki cha mvua kuwa inaendelea kufuatilia maeneo yote ambayo ni korofi na kuona namna nzuri ambayo inaweza kufanya ili kuwanusuru wananchi kuondokana na adha hizo na waweze kuendelea kupata huduma mbalimbali kwa kutumia barabara.
wananchi kuondokana na adha hizo na waweze kuendelea kupatahuduma mbalimbali kwa kutumia barabara.Kwandikwa amewahakikishia wananchi wa maeneo yote nchiniambao wameathiriwa na uharibifu wa mvua hizi katikamiundombinu ya barabara kurejeshewa kwa mawasiliano katikamaeneo hayo huku mwarobaini wa maeneo hayo koro2ukiandaliwa."Niwahakikishie wananchi kuwa Serikali yao iko makini,inasimamia rasilimali zote kwa makini na inakusanya fedha kwaajili ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi",amesema NaibuWaziri Kwandikwa.
Naye Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Matengenezo kutoka Wakalawa Barabara (TANROADS),mkoa wa Shinyanga MhandisiFrednand Mdoe, ameeleza kuwa wanapata changamoto kubwaya kurudisha mawasiliano katika barabara hiyo kutokana na majikuzidi kuongezeka na tayari washakusanya mawe kwa ajili yakurudisha barabara hiyo ili iweze kupitika."Huu ni mkondo wa Ziwa hivyo maji yamekuwa mengi na kuvukabarabara na kasi ya kupungua kwa maji haya imekuwa ndogolakini tumejipanga mipango ya sasa na mipango ya kudumuambayo ni ujenzi wa madaraja katika barabara hii katika mwakawa fedha unaokuja", amesema Mhandisi Mdoe.Naibu Waziri Kwandikwa yupo katika ziara ya kikazi mkoaniShinyanga ya kukagua athari za mvua zinazoendelea kunyeshahapa nchini na kusababisha uharibifu wa miundombinu yabarabara.
Post a Comment