UBUNGO, Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori ametembelea Kata za Kimara na Saranga ili kuona athari na kuwapa pole wananchi kutokana maafa yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo ya Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, juzi.
Mkuu wa Wilaya aliongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Diana Nkarage.
DC Makori aliwaambia wananchi wa Mtaa wa Golani Kata ya Kimara kuwa amefika kwao ili kujuliana hali na kuwapa pole wale wote walioathirika na mvua zilizonyesha Sikh ya Jumatano, tarehe 04/03/2020.
"Nimefika kwa niaba ya Serikali kuwapa pole wote ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine na mvua zilizonyesha hivi karibuni, nasema poleni sana.", Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya alisema kuwa amewasiliana na wadau mbalimbali ambao kama watakuwa tayari kusaidia basi Wilaya itaona namna ya kuwashika mkono.
Baada ya kutoka Mtaa wa Golani Mkuu wa Wilaya alitembelea Shule ya Msingi Saranga iliyopo Kata ya Saranga ambapo kuna madarasa matatu na vyumba mbili za Walimu ambazo zote ziliyoezuliwa paa.
Mkuu wa Wilaya aliwahakikishia wanafunzi na walimu kuwa tayari kuna jitihada za haraka zinafanyika ili madarasa na nyumba hizo za walimu ziweze kukarabatiwa na hatimaye wanafunzi waweze kupata sehemu ya kusomea.
Post a Comment