Mkuu wa ujumbe wa Shirika la Afya Duniani uliopo hapa nchini amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakabiliana kwa dhati dhidi ya maambukizo ya virusi vya corona.
Richard Brennan Mkuu wa ujumbe wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini nchini ambao ulielekea katika mji wa Qum kusini mwa Tehran kwa ajili ya kuchunguza hali ya maambukizo ya virusi vya corona jana usiku alikutana na kufanya mazungumzo na Bahram Sarmast Gavana wa Qum na kueleza kuwa: Kesi ya kwanza ya maambukizo ya virusi vya corona nchini Iran iliripotiwa tarehe 19 mwezi Februari na kuanzia hapo Jamhuri ya Kiislamu imetumia uwezo wake wote kukabiliana na maambukizo ya virusi hivyo.
Richard Brennan jana Jumamosi alikuwa na kikao na waandishi habari hapa Tehran ambapo alieleza kuwa Wizara ya Afya ya Iran inapifa hatua katika mkondo sahihi na kuongeza kuwa: Kumepatikana mafanikio makubwa katika uwanja wa tiba na majaribio ya kutambua virusi vya corona na upashaji habari nchini Iran.
Kama ilivyotangaza Wizara ya Afya na Tiba ya Iran hadi kufikia sasa watu 1,669 miongoni mwa walioambukizwa virusi vya corona hapa nchini wamepata nafuu.
Post a Comment