Featured

    Featured Posts

JAJI KIONGOZI ATAKA KESI ZA JINAI KUSIKILIZWA MFULULIZO


Na Magreth Kinabo- Mahakama
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Eliezer Feleshi amewataka Mahakimu kusikiliza kesi za jinai kwa mfululizo ili kuweza kupunguza msongamano wa mahabusu, na kuepukana na maambukizi ya Virusi Corona.

Jaji Kiongozi alitoa agizo hilo leo mara baada ya kutembelea mahakama mbalimbali za Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya ukaguzi maalum.
 
“Anzeni kusikiliza kesi za jinia mfululizo, itasaidia tusiwe na msongamano wa mahabusu, na wale wanaostahili dhamana wapewe, hatua hii itatuwezesha kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, alisema Jaji Kiongozi.

Aidha Jaji Kiongozi amewataka watumishi wa Mahakama kuendelea kuepukana na vitendo vya rushwa na kuzingatia maadili ya kazi zao.

Dkt. Feleshi alizipongeza Mahakama za Mwanzo kutokuwa na mlundikano wa mashauri.

Jaji Kiongozi ameanza ziara ya ukaguzi maalum katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo inatarajiwa kumalizika Aprili 3, mwaka huu.

Katika ziara hiyo Jaji Kiongozi alikagua ujenzi wa ujenzi wa jengo la Kituo cha Mahakama Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) kilichopo Kinondoni. . pia alikagua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Mahakama ya Wilaya Kinondoni na Mahakama za Mwanzo za Sinza, Kinondoni,Kaw. Kimara, Magomeni na Kariakoo.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi (katikati) akikagua leo ujenzi wa jengo la Kituo cha Mahakama Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) kilichopo Kinondoni. Kituo hicho kinajumuisha Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mahakama Mwanzo, zikiwemo ofisi za wadau wote wa Mahakama.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi (kulia) na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam( kushoto) (katikati) akinawa mikono mara ikiwa ni hatua ya kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha vya ugonjwa wa Corona baada ya kuwasili leo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam. Jaji Kiongozi yuko katika ziara maalum ya kikazi kwenye Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam. 
Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kariakoo akitoa (kushoto)taarifa ya utendaji wa Mahakama hiyo kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi( ambaye hayupo pichani). Picha na Magreth Kinabo- Mahakama
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana