Featured

    Featured Posts

JE NI TIBA ZIPI NNE AMBAZO WHO INAZIFANYIA UTAFITI KUTIBU KORONA?


Kufikia tarehe 23 mwezi machi , zaidi ya watu 350,000 walikuwa wamembukizwa virusi vya corona katika mataifa 170 duniani huku watu 16000 wakiripotiwa kufariki.
''Mpango mahsusi wa kuokoa maisha'', hivi ndivyo shirika la afya duniani WHO linavyoelezea juhudu zake mpya za kukabiliana na virusi vya corona.
Kufikia tarehe 23 mwezi machi , zaidi ya watu 350,000 walikuwa wameambukizwa virusi vya corona katika mataifa 170 duniani huku watu 16,000 wakiripotiwa kufariki.
Na idadi hiyo inaendelea kuongezeka kila uchao.
Bila tiba ama chanjo ambayo imeonekana kukabili virusi vya covid-19 madaktari wanaweza kufanya kazi kupunguza makali ya dalili za ugonjwa huo.
Kwasababu hiyo , shirika la afya duniani lilianzisha mpango wa mshikamano 'solidarity' ambao unahusisha utafiti ambapo mataifa kumi yatafanyia uchunguzi jinsi dawa nne zinavyoweza kutibu covid 19.
Lengo ni kukusanya data zaidi kwa wakati mfupi ili badala ya kuanza kutengeneza dawa mpya , mchakato unaoweza kuchukua miaka kadhaa , washiriki wa utafiti huo wataona iwapo dawa hizo zinazotumika kukabiliana na magonjwa mengine zitaweza kuzuia makali ya virusi vya corona.
Na ijapokuwa baadhi ya dawa hizi zinapatikana sokoni , madaktari , wanasisitiza kwamba hazifai kutumiwa bila ya ushauri wa mtaalamu.
Argentina, Bahrain , Canada, Ufaransa, Iran, Norway, Afrika Kusini, Uhispania, Switzerland na Thailand wamejiunga kufanya utafiti huo ambapo wanatarajia kwamba wagonjwa wengi watashiriki.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Virusi vya corona vilianza kusambaa kufikia mwisho wa 2019
" Umuhimu wa utafiti kama huu ni kwamba unaweza kusajili wagonjwa kwa haraka kulingana na daktari George Rutherford'' , profesa wa takwimu za kibaiolojia katika chuo kikuu cha Carlifonia nchini Marekani.
"Iwapo kwa mfano nilikuwa nikifanyia majaribio haya katika maabara yangu , ningekuwa na wagonjwa wawili au watatu kwa siku, lakini kutokana na ushirikiano wa vituo kadhaa unaweza kuwa na wagonjwa 100 kwa siku'', anaongezea.
Hiyo ni njia bora ya kuweza kufanya kazi kwa haraka.
Ana Maria Henao Restrepo , mtafiti katika shirika la afya duniani WHO idara ya chanjo na kinga ya kibaiolojia anasema kwamba mradi huo unafanywa kwa haraka zaidi.
Kulingana na Henao, WHO linatarajia kuwa na nakala na data ya utafiti huo kuanzia wiki ya mwisho ya mwezi Machi.
Rutherford anasema kwamba iwapo hakuna ,matatizo ya kimpango ya utafiti kama huo yanaweza kutoa matokeo katika kipindi cha mwezi mmoja.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kuenea kwa virusi vya corona kumewafanya watu kutotembea
Sambamba na utafiti huo wa kimataifa , WHO imesema kwamba wanasayansi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia wanafanyakazi ya kutengeneza takriban chanjo 20 za virusi vya corona.

Utafiti wa matumaini

Ili kuanzisha utafiti huo, jopo la watalaam wa WHO lilichagua tiba nne ambazo wanazithamini kuweza kukabiliana na virusi vya corona.
Waliangazia mbinu iliotumika kama vile habari kuzihusu na upatikanaji wao.
Tiba hizo zina dawa mchanganyiko ambazo zimetumika kutibu Ebola, malaria au HIV.
Tiba hizo zitatumika bila mpangilio , ikitegemea upatikanaji wake katika kila hospitali kwa wagonjwa wa virusi vya corona.
Baada ya tiba kuanza , madatari watachunguza jinsi wagonjwa wanavyoendelea , ikiwemo siku watakazoondoka hospitalini ama iwapo atashindwa kupona.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Watu wamelazimika kuwa ubami wa mita moja katika maeneo ya umma
Rutherford anasema kwamba katika tafiti kama hizi , lengo ni kuanzisha tiba katika awamu za kwanza za ugonjwa kabla ya mgonjwa kuingia katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Daktari huyo anaunga mkono mradi huo wa solidarity , lakini anaonya kwamba kufanya kazi na vituo tofauti katika mataifa kadhaa wakati mmoja inaweza kusababisha ugumu fulani.
Tiba nne

1.Remdesivir:

Licha ya kutengenezwa ili kutibu Ebola dawa ya remdesivir haikuonekana kuwa nzuri. Hata hivyo, inaonekana kuwa na uwezo dhidi ya coronavirus kulingana na vipimo vya seli zilizopandwa katika maabara.
Pia kuna ripoti za kwamba imekuwa na faida kubwa kwa wagonjwa wa covid-19, lakini hiyo haitoshi kuthibitisha kuwa dawa hiyo ni nzuri.
''Kati ya dawa zilizojumuishwa katika mradi wa Solidarity, remdesivir "inaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na virusi vya corona katika vipimo vya maabara," Stephen Morse, mkurugenzi wa mpango wa magonjwa ya kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Columbia (EE) aliambia BBC.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hakuna tiba wala chanjo thabiti dhidi ya virusi vya corona kufikia sasa

2. Cloroquina/hidroxicloroquina

Chloroquine ilitumika kwa miaka mingi kutibu ugonjwa wa malaria hadi pale vimelea ambavyo husababisha ugonjwa huo vilipomea sugu dhidi ya dawa hiyo .
Iwapo inaweza kutibu, haimaanishi kuwa itafanya kazi dhidi ya Covid 19," anasema Rutherford.
Dawa hii inaweza kutumika kupitia kinywa lakini pia hutoa athari za maumivu kama yale ya kuumwa na kichwa, kuhisi kisunzi,, kupoteza hamu ya kula, kuumwa na tumbo , kuhara, kutapika na kutokwa na upele katika ngozi, kulingana na Maktaba ya Kitaifa ya Tiba nchini Marekani.
Hatari yake ni kwamba ni rahisi kuipata na muonekano wake katika habari kuhusiana na virusi vya corona umesababisha kesi za sumu kuripotiwa

3. Ritonavir na lopinavir

Mchanganyiko wa dawa hizi mbili umetumika kwa matibabu ya VVU.
Wataalam walioshauriwa na BBC wanakubali kwamba mchanganyiko huu haujaonyesha matokeo ya kutia moyo dhidi ya coronavirus.
"Lakini ni busara kujaribu tena," anasema Rutherford.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Vita dhidi ya janga la corona ni miongoni mwa vita vigumu zaidi ambavyo wanasayansi wamekabiliana navyo katika historia ya hivi karibuni

4. Ritonavir / lopinavir

Tiba ya nne kupimwa na Solidarity ni mchanganyiko wa ritonavir na lopinavir pamoja na interferon-beta, molekyuli ambayo husaidia kudhibiti uchochezi na imeonekana kuwa bora kwa wanyama walioambukizwa na ugonjwa wa kupumua wa Mashariki ya Kati (MERS).
Wataalam wanaonya kuwa ni muhimu kuwa waangalifu wakati zinapotumika kwani, ikiwa zinatumika katika hatua za mwisho mwisho , zinaweza kukosa ufanisi au hata kusababisha madhara zaidi kuliko faida kwa mgonjwa.
Sasa ni suala la wakati gani matokeo hayo yatapatikana kwa mradi huo wa Mshikamano, lakini kulingana na Morse ni 'hatua moja kubwa iliopigwa' .
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana