Korea Kaskazini imefyatua leo kile kilichoonekana kuwa ni makombora mawili ya masafa mafupi katika pwani yake ya mashariki, ikiwa ni jaribio la nne la aina hiyo katika mwezi huu wakati ulimwengu ukipambana na janga la virusi vya corona.
Taarifa ya pamoja ya Wakuu wa Jeshi la Korea Kusini imesema makombora mawili yalifyatuliwa kuelekea mashariki kutokea mji wa bandari wa Wonsan na kuanguka katika Bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Mashariki.
Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema makombora hayo hayakuvuka mipaka yake ya baharini au kufika katika kanda ya kipekee ya kiuchumi ya nchi hiyo.
Korea Kaskazini wiki moja iliyopita ilifyatua makombora mawili ya masafa mafupi.
Siku moja baadaye, chombo cha habari cha nchi hiyo yenye silaha za nyuklia kikatangaza kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alimtumia barua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ikielezea kwa kina mpango wa kukuza mahusiano.
Credit: DW
Post a Comment