Featured

    Featured Posts

MAENDELEO, USTAWI WA JAMII DAR WAPIGWA MSASA KUHUSU CORONA

 Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kutoka katika Kata za mkoa wa Dar es Salaam wakati wa ufungunguzi wa mafunzo kwa wataalam hao juu ya mapambano dhidi ya Virusi vya Corona nchini Machi 28, 2020.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW)
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi akizungumza jambo kwa maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jmaii kutoka katika Kata za mkoa wa Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa  mafunzo  kwa wataalam hao juu ya mapambano dhidi ya Virusi vya Corona nchini.
 Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (kushoto) akiagana na Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Temeke Bi.Lilian Mafore  mara baada ya kufungua mafunzo kwa maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kutoka katika Kata za mkoa wa Dar es Slaam juu ya mapambano dhidi ya Virusi vya Corona nchini katikati ni Kamishna wa Ustawi wa Jmaii Dkt. Naftali Ng’ondi  
Baadhi ya maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kutoka katika Kata za mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu wakati wa mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Wataalam hao juu ya kukabiliana na maambukizo ya Virusi vya Corona.

NA PRUDENCE CONSTINE DAR ES SALAAM


Maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii nchini wametakiwa kushiriki kikamilifu kutoa elimu kwa umma dhidi 

ya maambukizi ya virusi vya Corona ili kuepusha ongezeko la maambukizi ya virusi hivyo.



Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya 

Jamii, Dkt. John Jingu wakati akifungua mafunzo kwa maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii wa Kata za 

Mkoa wa Dar  Es Salaam yaliyofanyika katika Manispaa ya Temeke.

Dkt. Jingu amesema kuwa elimu kwa umma hasa katika ngazi ya Kata na mitaa inategemea zaidi maafisa 

Maendeleo na Ustawi wa Jamii ili kukabiliana na maabukizi.


"Kama tutatimiza wajibu wetu kwa jamii kwa kutanguliza maslahi ya taifa, Tanzania itaepuka maambukizi 

zaidi ya virusi vya Corona" alisema.

Dkt. Jingu alikiri kuona kazi kubwa inayofanywa na watendaji mbalimbali ikiwa ni pamoja kusambaza 

Vitakasa mikono na barakoa katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kupambana na maambukizi.

Akiwasilisha mada katika kikao hicho, Mtaalamu kutoka Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Tumaini 

Haonga aliwataka washiriki kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam ili jamii inayowazunguka ipate 

elimu sahihi.

 "Sio kila mwenye homa na kukohoa anachukuliwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona lazima 

mshukiwa aonyeshe sifa za ziada ama awe amesafiri kwenda au kutoka nje ya nchi iliyo na maambukizi, 

amechangamana na watu walioambukizwa au kuwahudumia  waathirika ndani ya siku 14 zilizopita" alisisitiza.

Kwa upande wake, Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Dkt. Naftali Ng'ondi amewataka maafisa hao kujiepusha na 

misongamano isiyo ya lazima ili kuepusha maambukizi katika maeneo yao.

"Kama ni kwenda sokoni, hakuna sababu ya kuandamana watu wanne wa familia moja na tunapokwenda 

sokoni twende kimkakati" alisema.


Aliongeza kuwa maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii wanawajibika kuwaelimisha wananchi juu ya madhara 

ya msongamano hasa kwa kipindi hiki wakati wa tishio la virusi vya Corona. 

Mgonjwa wa  kwanza aliripotiwa nchini Tarehe 16 Machi, 2020 na hadi sasa watu 13 wamethibitika kupata 

virusi vya Corona.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana