Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na washitakiwa wenzake wakiwa Mahakamani leo. Mwenye nguo nyeusi ni Maalim Seif Sharif Hamad.
KISUTU, Dar es Salaam
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam, imewatia hatiani viongozi wanane wa Chadema na Katibu Mkuu wa zamani wa chama hicho Dk. Vicent Mashinji, katika mashtaka 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili, isipokuwa shtaka la kwanza la kula njama.
Akisoma hukumu kwa washtakiwa hao, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Thomas Simba, amewahukumu kila mmoja kulipa faini ama kwenda jela miezi mitano.
Katika shtaka la pili kila mshtakiwa ametakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 10 au kwenda jela miezi mitano, shtaka la 3 hadi la 6, kila mshtakiwa ametakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 10 au kwenda jela miezi mitano, ambapo katika shtaka la nane, Mbunge John Heche amekutwa na hatia na kutakiwa kulipa faini ya sh. milioni 10 au kwenda jela miezi mitano.
Aidha Wabunge John Mnyika, Salum Mwalimu, Ester Matiko na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Vicent Mashinji, kila mmoja ametakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 30, na huku, John Heche, Peter Msigwa, Halima Mdee na Ester Bulaya wakitakiwa kila mmoja kulipa Milioni 40.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, yeye ametakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 70 au kwenda jela miezi mitano.
Post a Comment