Featured

    Featured Posts

MAJALIWA: TUTAHAKIKISHA CORONA HAISAMBAI ZAIDI NCHINI, AVISHUKURU VYOMBO VYA HABARI KWA KUELIMISHA UMMA NAMNA YA KUJIKINGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu   kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini, kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, leo, Machi 23, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)














DODOMA, Tanzania
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kufanya tathmini ili kuhakikisha inazuia ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona isiweze kusambaa kwa kiasi kikubwa nchini, huku akivishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano vinaoutoa kwa Serikali katika kuelimisha umma namna ya kujikinga na virusi vya ugonjwa huo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Machi 23, 2020, wakati akizungumza na Mawaziri na Makati Wakuu katika Kikao Kazi cha mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma.

Katika kikao hicho umewekwa mkakati kuwa kinga dhidi ya virusi vya Corona iwe ni jambo la kimkakati zaidi kuliko kusubiri kutibu, hivyo kwa sasa Serikali imeweka mkazo kwenye kuwahamasisha wananchi kujikinga na virusi hivyo.

“Mawaziri hakikisheni katika kipindi hiki ziara za kwenda kukagua miradi zielekezwe kwa Wakurugenzi ikibidi kwa Makatibu Wakuu, Mawaziri mnatakiwa mjikite katika kukinga Taifa na ugonjwa huu wa corona", amesema Waziri Mkuu akiwaangiza Mawaziri.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeunda Kamati tatu kwa ajili ya kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi ya corona (COVID-19) ambazo kamati hizo ni ya Kitaifa ambayo itaongozwa na Waziri Mkuu na itahusisha baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Kamati ya pili ni ya Makatibu Wakuu  kutoka sekta husika na itaongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi na kamati ya tatu ni ya Kikosi Kazi cha Taifa ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto huku wajumbe wake wakiwa ni wataalamu akiwemo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mapema, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema katika kipindi cha saa 24 jumla ya watu 292,142 duniani walibainika kuwa na virusi vya Corona kati yao watu 12,784 wamefariki, huku katika Bara la Afrika wakiwa ni watu 736 waliobainika kuwa na virusi vya Corona na kati yao watu 20 wamefariki katika kipindi cha saa 24.

Kwa upande wa Tanzania, Waziri Ummy alisema jumla ya watu 12 walibainika kuwa na virusi vya Corona tangu mgonjwa wa kwanza alipogundulika nchini na kwamba wagonjwa wote hali zao ni nzuri na mmoja amepimwa zaidi ya mara mbili na kubainika kuwa hana virusi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana