Mbunge wa Wawi Mkoa wa Kusini Pemba (CUF), Ahmed Juma Ngwali (mwenye flana nyekundu) amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ngwali ametangaza uamuzi huo leo Jumatatu Machi 2, 2020 mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ambaye yupo Zanzibar katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilaya za kisiwani Pemba.
Mbunge huyo amesema anajiunga CCM kwa sababu chama hicho tawala kinapeleka maendeleo kwa wananchi.
Ngwali anaungana na wabunge wengine wanne wa CUF waliojiunga CCM ambao ni Maulid Mtulia (Kinondoni), Ahmed Katani (Tandahimba), Abdallah Mtolea (Temeke) na Zuberi Kuchauka (Liwale).
Post a Comment