Featured

    Featured Posts

MSAIDIZI WA NETANYAHU ATHIBITIKA KUWA NA VIRUSI VYA CORONA

   Msaidizi wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amethibitika kuwa na virusi vya Corona, maafisa wamesema leo, lakini haijafahamika mara moja iwapo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 70 ameambukizwa ama kazi yake itaathirika.
 Afisa mmoja wa serikali amesema kuwa hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa maelekezo ya wizara ya afya, na kusema msaidizi huyo wa bunge ambaye vyombo vya habari nchini Israel vimemueleza kuwa yuko katika hali nzuri, atafanyiwa uchunguzi.

 Kwa kawaida wizara ya afya inataka kutengwa kwa mtu anayeshukiwa kuwa na maambukizi kwa muda wa siku 14 na kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya corona mtu yeyote anayeonekana kuwa alikuwa karibu na mtu aliyeambukizwa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana