SINGIDA,Tanzania
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekabidhi mifuko 30 ya saruji ikiwa ni namna ya kuunga mkono ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoawa Singida.
Ujenzi huo ni mpango wa jumuiya hiyo wa kuhakikisha wanajenga nyumba za watendaji wao kwa kila mkoa nchi nzima.
Akikabidhi mchango huo machi 28 Mtaturu amewapongeza UVCCM chini ya Mwenyekiti wake Kheri James kwak uja na mpango huo wenye lengo la kuwapa makazi ya kudumu watendaji wake.
“Mpango huu ni mzuri sana,niwapongeze UVCCM na viongozi wenu kwa kuweka mikakati inayoacha alama,nimekabidhi mifuko hii ya saruji 15 lakini pia ninachangia pesa ya kuwalipa mafundi sh 80,000 na ninawaahidi kuendelea kuwaunga mkono katika jambo hili jema mnalolifanya,”alisema Mtaturu.
Amewapongeza UVCCM mkoa wa Singida chini ya mwenyekiti wake Dkt Denis Nyiraha kwa kuweka Mpango wa Utekelezaji wa maazimio ya Taifa ambapo kwa sasa wapo mbioni kumaliza nyumba ya Katibu wa Mkoa ili hatimaye waendelee kusimamia kwa ngazi za Wilaya.
“Hii ndio tofauti ya CCM na vyama vingine vya mfukoni ambavyo hata Ofisi havina,hivyo hawawezi kuwa na Mpango huu ambao unafanywa tu na Jumuiya ya vijana ya CCM,”aliongeza Mtaturu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Dkt Nyiraha amemshukuru mbunge Mtaturu kwa utayari wake wa kuunga mkono mpango wa Ujenzi wa nyumba ya mtendaji wa Uvccm Mkoa.
“Kwa niaba ya jumuiya hii mkoa nitoe shukrani zetu kwako,tunatambua siku zote kila tunavyokufikia kwa mambo mbalimbali yanayohusu Jumuiya yetu umekuwa mwepesi sana,”alisema.
Katibu wa UVCCM Mkoa George Silindu amesema hiyo ni heshima kubwa kwa watendaji kupatiwa makazi yenye heshima yatakayoleta utulivu na kuongeza ari ya kazi.
“Matarajio yetu hadi kufikia mei,2020 nyumba hii iwe imekamilika ili Mkoa ushuke kusimamia ujenzi ngazi ya wilaya ambao utagharimu sh milioni 25 kwa nyumba moja,”alisema Silindu
Post a Comment