Papa Francis amekubali kujiuzulu kwa Kadinali wa Ufaransa Philippe Barbain, ambaye alikutwa na hatia na kisha kuondolewa mashitaka kwa kushindwa kuripoti madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto.
Kadinali Barbain wa Lyon mwenye umri wa miaka 69, aliomba kujiuzulu wakati mahakama ya Lyon ilipomtia hatiani kwa mara ya kwanza mnamo Machi 2019, na kumpa adhabu ya kifungo iliyoahirishwa kwa miezi sita.
Barbain alituhumiwa kushindwa kumripoti Padri Bernard Preynat polisi hata baada ya kufahamu matendo yake.
Papa Francis alikataa ombi hilo wakati huo, akisema anasubiri matokeo ya rufaa. Alimruhusu askofu huyo kukaa kando na kukabidhi majukumu yake ya kila siku kwa kaimu wake.
Padri Bernard Preynatt alikiri kuwanyanyasa watoto kingono katika miaka ya 70 na 80.
Post a Comment