Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad kwa kutokugusana mikono, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Salamu hiyo ya kutokugusana mikono ni kutekeleza ushauri ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wenye lengo kujihadhari dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo ya faragha na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment