Featured

    Featured Posts

RAIS MAGUFULI: WATANZANIA NA WAGENI WATAKAOINGIA NCHINI KUTOKA NCHI ZILIZOATHIRIWA NA CORONA WOTE KUJITENGA SIKU 14 KWA GHARAMA ZAO.

Rais Dk. John Magufuli akihutubia Taifa katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Machi 22, 2020

IKULU, Chamwino, Dodoma
Rais Dk. John Magufuli leo ametangaza hatua nyingine ili za kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Coron

Rais Dk. John Magufuli amesema kuanzia kesho wasafiri wote watakaoingia nchini kutoka katika mataifa yaliyoathirika zaidi na ugonjwa wa Corona, watalazimika kufikia sehemu za kujitenga kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe.

Akihutubia taifa, mchana huu, Rais Dk. Magufuli amefafanua karantini hiyo ya kufikia sehemu za kujitenga kwa siku 14 kwa gharama zao, itawahusu pia Watanzania wanaotoka kwenye nchi hizo ambao walikwenda kwa shughuli mbalimbali.

"Naelekeza Wizara ya Afya pamoja na Mamlaka nyingine husika, kuhakikisha maabara ya taifa inaimarishwa kwa kupatiwa vifaa vya kisasa vya uchunguzi. Aidha Naagiza Maeneo yote ya vituo yanatotumiwa na watu  kuingia nchini yapelekewe vifaa vya ukaguzi na pia vya kujikinga kwa ajili ya watumishi. 

Katika hilo navihimiza pia vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu yote ili kuzuia watu kuingia nchini koholela bila kufanyiwa uchungizi", amesema Rais Dk. Magufuli.

"Seriakli kuanzia sasa imesitisha kutoa vibali vya usafiri kwa watumishi kwenda kwenye nchi zilizoathirika na ugonjwa huo wa Corona. Aidha tunawasihi na kuwashauri wananchi ambao hawana shughuli za lazima sana za kutembelea nchini hizo pamoja na maeneo mengine yakiwemo ya ndani ya nchi kuahirisha safari zao kwa sasa", amesema Rais Dk. Magufuli.

Rais Dk. Magufuli amesema ili kuimarisha mikakati ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo, serikali imeunda  Kamati ya kupambana na ugonjwa ambayo itakuwa chini ya Waziri Mkuu akisaidiwa na Waziri wa afya na wajumbe wengine watachaguliwa na Waziri Mkuu kutokana na umuhimu wao.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana