Na Mwandishi Maalum, Simiyu
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto hasa wa kiume ambao baadhi wamekuwa wakiwadhalilisha kwa kuwalawiti.
Ameyasema hayo leo mkoani Simiyu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani hapa/
Makamu wa Rais amewataka Watanzania kusimama pampja kwa kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie na kuwa katika mapambano hayo ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
"Sasa hii tabia ya kuwageuza watoto wa kiume tunatengeneza taifa gani la kuwaharibu watoto hawa na pia mjue kusema hili siyo luwapa uhalali kuwafayia vitendo hivyo watoto wa kike" alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amezitaka Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto kufanya kazi na kuacha mambo ya kujuana ili Sheria ichukue mkondo wake pale inapotokea mtu amefanya kitendo cha kikatili.
Ameisisitiza kuwa jamii ni lazima kusimama pamoja katika kupinga na kupambana na vitendo vya ukatili katika maeneno yao kwani vitendo vingi hufanywa na watu wa karibu na familia hivyo huvifumbia macho na waathirika wa vitendo hivyo kukosa haki zao.
Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa agemda ya usawa wa kijinsia sio ya wanawake peke yao ila ni ya kwa wote yani wanawake na wanaume ili kuweza kuleta usawa wa kijinsia.
Ameongeza kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa chachu kwa watoto wa kike na wanawake wa Tanzania katika kuwaza makubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii ya kijinsia.
"Tunamshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa fursa wanawake katika uongozi na hakika hatujamuangusha tumezitendea haki nafasi zetu" alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa utaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu na kuwa na maendeleo kwani mtazamo na elimu itamsaidia mtoto wa kike katika kupambanua mambo na kujiletea maendeleo.
"Tukiweza kumsaidia mtoto wa kike kufika katika maendeleo yake ni kumsaidia kuondokana na changamoto zinazomkwamisha kufikia malengo yake" alisema
Ameongeza kuwa muhimu ni kwa wadau kushirikiana na Serikali kuwezesha mabweni yatakayosaidia watoto wa kike kuondokana na vishawishi vitakavyowasababishia kuwarudisha nyuma katika kufikia ndoto zao.
Mtaka amewataka wazazi na walezi kuzingatia elimu ya jinsia kuanzia kazi ya familia ili kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia kuanzia katika familia ili kuweza kumkomboa mtoto wa kike na ukandamizaji na unyanyasaji.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake yamefanyika Kitaifa katika mkoa wa Simiyu yakiwa na Kauli Mbiu 'Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na Baadaye'.
Post a Comment