Featured

    Featured Posts

TAMISEMI YAIJENGEA UWEZO KAMATI YA LISHE MANISPAA YA UBUNGO KWA MAFUNZO JINSI YA KUINUA KIWANGO CHA LISHE

Mafunzo hayo  yamefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya uliopo Luguruni na kuhudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Das Wilaya ya Ubungo Diana K. Nkarage. Mkufunzi alikuwa ni  Mratibu wa  lishe kitaifa kutoka OR  TAMISEMI Ndg. Mwita Waibe akisaidiwa na Afisa Lishe wa Mkoa wa Dar es salaaam Neema Kweba, Dr.Winfrida Mayilla Senior Program Manager kutoka Shirika la GAIN na Afisa Lishe wa Wilaya ya Ubungo Beatrice Joseph pamoja na  wataalam kutoka Manispaa ya Ubungo.

Lengo la mafunzo likiwa ni kuzijengea uwezo kamati za lishe pamoja na wafanya maamuzi (Wakuu wa Wilaya) kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi za  Kata na Mtaa/vijiji na Kutambulisha nyenzo na kukusanya taarifa za utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe ngazi ya Kata na Mtaa/vijiji.

*"Tuzingatie lishe katika maisha yetu kwa kuhakikisha tunakula vyakula ambavyo vina virutubisho sahihi(vyakula vyenye lishe bora) na kuepukana na madhara ambayo yanaweza kutokea na kuleta hasara kiuchumi, katika ngazi ya familia mpaka Taifa kwa kukosa kizazi chenye ukuaji mzuri. Pia Udumavu huathiri ukuaji wa mwili hata akili kwa Tanzania tafiti zinaonyesha ina watoto waliodumaa takribani millioni 3 ambayo ni sawa na 31.8%*

*Ili kuepukana na janga la watoto wadumavu na kizazi cha watu wenye ukuaji mbovu wa mwili lazima siku 1000 za ukuaji wa mtoto uzingatiwe."* Alisema hayo  Mratibu wa Lishe Ndg. Mwita

"Pia kuwekeza kwenye Lishe ni jambo muhimu tuige mfano mzuri kutoka nchi za wenzetu kumekuwa na ongezeko kubwa la kizazi chenye ukuaji mzuri wa afya ya akili ambao tumekuwa tukiwategemea katika mambo mbalimbali ili  kupata wafanisi wakubwa, tujielekeze sasa kuinua watoto kwa kuwapa lishe bora  walio katika Wilaya yetu na  kwa kutoa elimu bora kuhusu lishe kwa wazazi." Aliongeza Ndg. mwita

Aidha mwakilishi kutoka Shirika la GAIN *Dr. Winfrida Mayila* ambaye ndiye Senior Program Manager wa Shirika la GAIN  aliomba kamati kuainisha mahitaji yao na GAIN   itachangia  kiasi cha Tsh. Millioni  30 ili  kuisaidia kamati  kuinua swala la lishe katika Wilaya ya Ubungo.

Ikumbukwe kuwa GAIN ni Shirika lisilo la kiserikali linaloshirikiana na Serikali ili kusaidia afua mbalimbali za lishe katika kutekeleza mkataba wa lishe ambao wakuu wa Mikoa wamesaini pamoja na Wilaya zote.

Mwisho Kaimu Das Wilaya ya Ubungo aliwashukuru wawezeshaji kutoka Tamisemi kwa ujio wao na kutoa elimu kuhusu lishe na kuwakaribisha tena Manispaa ya Ubungo.

IMETOLEWA NA
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO MANISPAA YA UBUNGO
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana