ROME, Italia
ITALIA imeamua kuwatumia wanajeshi ili kuongeza nguvu ya kuzuia watu kutoka nje, Jana, Ijumaa Machi 20, 2020, huku maafisa wakisema watu 627 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona katika kipindi cha saa 24.
Idadi hii ya vifo ndiyo kubwa zaidi kutokea ndani ya siku moja duniani tangu mlipuko wa ugonjwa huu utokee nchuni China.
Kupoteza matumaini kwa baadhi ya watu kumeanza kuonekana Kaskazini mwa nchi hiyo hususan kwenye jimbo lililloathirika zaidi la Lombardy ambako kwa mara ya kwanza mlipuko wa ugonjwa huo uliripotiwa mwezi mmoja uliopita.
Wataalamu wa tiba kutoka China ambao wametua nchini Italia kutoa usaidizi kutokana na uzoefu wao wa kukabiliana na maradhi hayo wamesema, makatazo mbalimbali yaliyotolewa ili kukabiliana na ugonjwa huo hayakuwa na nguvu za kutosha.
Hatimaye sasa serikali imekubali kuweka wanajeshi ili kusaidia utekelezaji wa makatazo hayo yakiwemo ya watu kutokutoka nje ya nyumba zao,
"Ombi la kuwatumia Wananjeshi kwenye operesheni hii limekubaliwa, na wanajeshi 114 watakuwa mitaani kwenye mkoa wote wa Lambardy.” Amesema Rais wa mkoa wa Lambardy, Attillio Fontana kuwaambia waandishi wa habari..
Hadi sasa zaidi ya watu 4,000 wamefariki dunia nchini Italia kutokana na ugonjwa huo, Shirika la kuwahami wananchi (Civil Protection Agency) la nchi hiyo limesema, watu wengine wapya 6,000 wamethibitika kuwa na maambukizi ya Corona na hivyo kufanya idadi ya jumla kufikia 47,000.
@ Rome, Italy
Post a Comment