Featured

    Featured Posts

WHO: MAJARIBIO CHANJO YA COVID-19 (CORONA) YAMEANZA

WHO: Majaribio ya chanjo ya COVID-19 (Corona) yameanza
Shirika la Afya Duniani limesema siku 60 baada ya sampuli za virusi vya Corona au COVID-19 kuwasilishwa na China, chanjo ya kwanza ya majaribio imeanza.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema, “haya ni mafanikio makubwa, tunawapongeza watafiti kote duniani ambao wamekuja pamoja ili kutathmini majaribio ya tiba."
Ameongeza kuwa WHO na washirika wake wanaandaa utafiti katika nchi nyingi ambako baadhi ya nchi hizo dawa hizi ambazo hazijajaribiwa zitalinganishwa.
Amesema utafiti huo mkubwa unaandaliwa ili kukusanya takwimu zinazohitajika kuonyesha matibabu yapi yanafaya kazi zaidi.
Dkt. Tedros amesema mchakato huo umepewa jina la “Majaribio ya Mshikamano”.
Mkurugenzi huyo mkuu wa WHO amesema tayari nchi kadhaa zimethibitisha kwamba zitashiriki utafiti huo wa  "Mshikamano wa Majaribio" zikiwemo Argentina, Bahrain, Canada, Ufaransa, Iran, Norway, Afrika Kusini, Hispania, Uswisi na Thailand na amesema anaamini nchi nyingine nyingi zitajiunga.
Daktari Tedros ameongeza kuwa mfuko  wa hatua za mshikamano dhidi ya COVID-19 hadi sasa umeshakusanya zaidi ya dola milioni 43 kutoka kwa watu zaidi ya 173,000 na mashirika ikiwa ni siku chache tu tangu ulipozinduliwa.
 Amesisitiza kwamba virusi hivi ni tishio kubwa lakini pia ni fursa ya kuja pamoja kukabiliana na adui huyu mkubwa dhidi ya ubinadamu.
Mkurugenzi mkuu wa WHO amesema hadi sasa watu zaidi ya 200,000 wameambukizwa COVID-19 duniani na miongoni mwao zaidi ya 8,000 wameaga dunia.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana