Mabilioni ya watu kote duniani kwasasa wanasalia nyumbani kwasababu ya virusi vya Corona - jambo ambalo linabadilisha mwenendo wa dunia.
Kwasababu ya amri ya kutotoka nje wanaokwenda kazini ama kutumia usafiri wa reli au wa barabara ni kidogo mno huku kampuni nyingi zikiwa zimefungwa.
Ukweli ni kwamba, idadi kubwa ya watu wanafanyakazi kidogo tu kuliko vile inavyotarajiwa na hilo limepunguza mitikisiko katika tabaka la juu la dunia.
Hii ni habari njema hasa ukizingatia kwamba dunia ina uzito wa tani trilioni bilioni sita.
Kupungua kwa kiasi kikubwa
Wanasayansi nchini Ubelgiji walikuwa wa kwanza kubaini hili, na kusema kwamba mitikiso ya ardhini imepunga sana tangu kuanzishwa kwa hatua za amri ya kutotoka nje katika baadhi ya mataifa duniani.
Mabadiliko hayo pia yametambuliwa katika maeneo mengine duniani.
- Coronavirus: Kwa nini ni hatari kugusa uso wako
- Jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona
- Majibu ya maswali 10 yanayoulizwa sana kuhusu coronavirus
Mtaalamu mmoja wa masuala ya matetemeko ya ardhi, mfanyakazi katika Taasisi moja ya masuala ya ardhini amesema mitikiso ya ardhini katika mji mkuu wa Ufaransa umepungua sana, huku Marekani mitikiso hiyo ikisemekana kupungua hata zaidi kulingana na utafiti wa chuo kikuu cha Cal Tech.
Hali safi ya hewa na bahari tulivu
Hii sio njia pekee ambayo virusi vya corona vimebadilisha maisha ya kila siku kote duniani.
Setilaiti zimebaini kupungua kwa uchafuzi wa mazingira kunakosababishwa na gesi ya naitrojeni dioksaidi, ambayo chanzo chake ni magari, malori, mabasi na viwanda vya kuzalisha umeme.
Dunia imenyamaza mno.
Mwanasayansi ambaye hupima kiwango cha kelele katika miji mbalimbali kila siku na wale watafiti wa kina cha bahari wanasema kwamba kiwango cha sauti kimepungua.
Mawimbi mazuri
Utafiti mpya wa matetemeko ya ardhi hakumaanishi kwamba dunia imeacha kutikisika kabisa, lakini mabadiliko hayo siyo tu kwamba yanashuhudiwa na wanasayansi lakini pia ni muhimu sana kiuhalisia.
Shughuli za binadamu ni kama kelele za chinichini ambako kunafanya iwe vigumu zaidi kusikiliza uhalisia wa kinachokea ardhini.
“Utapata ishara ambayo haina kelele sana ambayo inawezesha kupata taarifa kidogo,” mtaalamu wa matetemeko Andy Frassetto kupitia mtandao, ameelezea katika Taasisi za Utafiti wa matetemeko ya ardhi mjini Washington.
Baadhi ya watafiti wamefanikiwa kuzungumzia kile hasa kile kinachosababisha kupungua kwa mitikiso ya chini ya ardhi.
Stephen Hicks, kutoka chuo cha Imperial College London, amesema kwamba kupungua kwa mitikiso ya chini ya ardhi katika eneo lake kumetokana na kupungua kwa msongamano wa magari kati ya London na Wales.
“Ni wazi kwamba katika siku chache zilizopita, kiwango cha kelele alfajiri kimepungua kuliko siku za nyuma,” ameandika kwenye mtandao wa Twitter.
Nadhani hili ni kwasababu hakuna tena msongomano wakati wa asubuhi huku idadi ndogo tu ya watu ikiwa ndo inayoabiri usafii uliopo na shule pia zimefungwa.”
Mabadikilo ya muda
Mabadiliko haya yana chanzo chake.
Bila shaka shughuli za binadamu hutofautiana kila siku kwasababu pia kuna wakati ambao shughuli hupungua.
Usiku huwa ni tulivu ikilinganishwa na mchana na kupungua kwa mitikiso namna hii hutokea wakati wa sikukuu kubwa au matamasha.
Lakini kile kinachotokea kote duniani ni kupungua kwa shughuli kwa wiki kadhaa, au miezi tukio ambalo hushuhudiwa wakati wa sikuu ya Krismasi katika nchi za Kikiristo.
Post a Comment