Featured

    Featured Posts


Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linafanya msako mkali kumtafuta HAKIMU JAMES MWAKIFUNA miaka [20] Mnyakusa wa Kiwira kwa kosa la Mauaji ya makusudi ya bibi JUNE SANKANYE miaka [65] wa kijiji cha Nkunga Kata ya Nkunga  {T} Ukukwe.

Tukio hili lilitokea tarehe 23/04/2020 saa 05:00 Wilaya ya Rungwe.  Marehemu ambaye ni bibi mzaa baba wa mtuhumiwa walilala nyumba moja.  Huku mtuhumiwa akiwa sebuleni na marehemu amelala chumbani.   

Usiku muda usiojulikana HAKIMU JAMES MWAKIFUNA alichukua kitu chenye ncha kali na kumkata bibi shingo na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili na kisha kuondoka na kichwa cha JUNE SANKANE.

Mnamo tarehe 18/04/2020 mtuhumiwa HAKIMU J. MWAKIFUNA alianza kuvua nguo na kutembea na Panga huku akitaka kuua baadhi ya ndugu zake aliokuwa akiishi nao Kiwira kwa bibi mzaa mamaye – MONICA BUKUKU.  Kufuatia hali hiyo tarehe 21/04/2020 alifukuzwa na kwenda kwa marehemu ambaye ni bibi yake mzaa baba yake.

Baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa alitoboa ukuta wa nyumba ya marehemu na kuondoka na kichwa kwenda kusikojulikana.

Jeshi la Polisi linatoa rai ni tukio baya sana kutokea mkoani kwetu na kuwasihi wananchi na viongozi wote wa wananchi popote akionekana mtu mwenye dalili za upungufu wa akili apelekwe hospitali kupata matibabu.
 
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana