Featured

    Featured Posts

MCHEKESHAJI PIERRE LIQUID AKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA

Msanii wa Maigizo na Mchekeshaji 'Pierre Liquid' amethibitisha kuwa na virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya Mapafu
Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti la Mwanaspoti Pierre amesema kwa sasa yupo hospitali ya Amana akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.

Akieleza namna alivyogundulika kuwa ana corona,amesema hii ni baada ya kwenda kupima wiki iliyopita hospitali ya Temeke. "Nina bosi wangu wa karibu ambaye kapata ugonjwa huu na kwa kuwa mara nyingi tuko naye alinishauri na mimi nikapime kwa nia njema ili kama ninao nipate matibabu mapema na kuepuka kuwaambukiza wengine. " Hivyo nilienda hospitali ya Temeke, wakanipima ndipo nilipokutwa ninao na kuletwa hapa Amana ambapo kwa sasa ni moja ya kituo cha wagonjwa,"amesema Pierre.

Alipoulizwa anadhani ni wapi kaupatia,
amesema "Huu ugonjwa mimi nitakuwa nimembukizwa nikiwa baa hakuna sehemu nyingine kwa kuwa ndio maeneo yangu ya kujidai,". Source : Mwanaspoti
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana