Featured

    Featured Posts

MUFTI MKUU SAUDI ARABIA ATANGAZA TARAWEHE NA IDDI KUSWALIWA MAJUMBANI

  Mufti Mkuu wa Saudi Arabia, Sheikh Abdulaziz Al-Sheikh, amesema kuwa sala zote kwenye mwezi wa Ramadhan na Eid-al-Fitr zitapaswa kuswaliwa majumbani, endapo janga la kirusi cha corona litaendelea, hii ikiwa fatwa ya karibuni kabisa kutolewa na kiongozi huyo wa juu wa dini ya Kiislamu nchini humo.

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unaanza wiki ijayo, katika wakati ambapo maradhi ya COVID-19 yakipamba moto. Katikati ya mwezi uliopita wa Machi, Saudi Arabia ilifunga misikiti yote kuzuwia mikusanyiko ya swala za jamaa, ili kujikinga na mripuko wa virusi vya corona.


Jana, Alkhamis, Msikiti wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani Ziwe Juu Yake) katika mji mtukufu wa Madina, nao ulitangaza marufuku ya mikusanyiko yote ya mwezi wa Ramadhani, ikiwemo futari ya pamoja, chakula cha kwanza kwa waumini wa Kiislamu wanaofunga, ambacho kwa aghlabu huliwa kwa pamoja baada ya jua kuzama.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana