Wakuu wa nchi 20 zenye nguvu kiuchumi na zinazoinukia kiuchumi duniani, G20 wamekubaliana kusamehe kwa muda madeni ya nchi masikini duniani.
Mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa G20 wamesema wanaunga mkono kusimamisha kwa muda malipo ya madeni kwa nchi hizo ambazo zinahitaji kuvumiliwa.
Uamuzi huo umefikiwa jana katika mkutano wao uliofanyika kwa njia ya video.
Muda huo unaanza Mei Mosi hadi mwishoni mwa mwaka 2020 na deni kuu pamoja na malipo yote ya riba yatasimamishwa.
Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani, IMF Kristalina Georgieva ameupongeza uamuzi huo.
Katika taarifa yao ya pamoja IMF na Benki ya Dunia zimesema zimefurahishwa na hatua hiyo ya G20 ya kuitikia wito wao wa kiziruhusu nchi masikini duniani ambazo ziliomba kuvumiliwa na kusimamishwa kwa muda ulipaji rasmi wa madeni yao kuanzia tarehe moja ya mwezi Mei.
Post a Comment