Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MFANYABIASHARA maarufu nchini Rostam Aziz amekabiodhi vifaa mbalimbali vikiwamo vitakasa mikoni na barakoa ili kusaidia mapambano dhidi ya Corona jijini Dar es Salaam.
Rostam amekabidhi msaada huo leo Aprili 16 mwaka 2020 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwa Waziri Mkuu aliyoitoa wiki iliyopita ya kutoa Sh.bilioni moja kusaidia vifaa hivyo katika daladala za jiji la Dar es Salaam na Zanzibar.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Rostam amesema pamoja na vitakasa mikono hivyo na barakoa alizotoa lakini leo ameongeza mchango wake kwa hospitali mbalimbali kwa wauguzi wote ambapo amejitolea barakoa 70,000 ili madaktari na manesi ambao ndiyo wako hatarini kuliko mtu yeyote.
Vingine ni galoni 6,000 za lita tano za vitakasa mikono na mashine maalumu za kupuliza dawa ya kupambana na maambukizi ya virusi hivyo.
“Kama nilivyosemna tuna janga. Janga hili la maradhi ya Corona haliko tu Tanzania lakini lipo sehemu zote duniani. Na kama sote tunavyojua ugonjwa huu hauna tiba, tiba pekee ni kujihami usiupate.
“Mheshimiwa Rais wetu Machi 22 mwaka huu, katika hotuba yake kwa taifa kuhusu janga hili, akitangaza maradhi ya Corona alitupa tahadhari , alituambia pamoja na kuchapa kazi na kuendelea na shughuli zetu za kila siku za kutafuta riziki lazima tuchukue tahadhari kwa kunawa mikono, kutokusanyika na mengineyo.
“Hivi sasa ni wazi kwamba tahadhari hizo inabidi tuzizingatie kuliko wiki iliyopita au wiki mbili zilizopita, leo hii kwa mara ya kwanza nimevaa hii kitu inaitwa barakoa na hii nimetengenezewa na mama yangu kwa hiyo huna haja ya kwenda kuinunua dukani unachukua shuka au foronya unaifunga na kamba,” amesema Rostam.
Akizungumza namna barakoa hiyo inavyofanya kazi, Rostam amesema inaweza kukuepusha na maradhi mengi, na kwamba jambo hilo linaweza kufanyika kwa kila mtu ambapo unaweza kuchukua nguo yako iliyochakaa ukatengeneza.
Amesema amezungumza na madktari wakamwambia ni vema kuvaa barakoa wakati unakwenda kwenye msongamano wa watu lakini pia watu wanaweza kutengeneza wenyewe si lazima kununua madukani.
Pamoja na mambo mengine, Rostam ametoa wito kwa wafanyabiashara wengine kuisaidia serikali kwa kutoa msaada wa vifaa vya kupambana na corona akitolea mfano kwa nchi nyingine wafanyabiashara walivyosaidia nchi zao
“Kama kawaida yangu ningependa kuwaomba wafanyabiashara wenzangu hili si jukumu la serikali pekee, wafanyabiashara wengi duniani wameishaidia serikali, tumeona Amazon wamejitolea. Si lazima uwe mfanyabiashara mkubwa, hata mfanyabiashara wa duka unaweza kuweka ndoo ya maji dukani na ukaweka vitakasa mikono kwa wafanyakazi unaweza kuokoa maisha ya watu.
“Natoa mwito kwa wafanyabisahrawa wakubwa na wadogo kwa kikasi tunachoweza tusaidiane kuisaidia serikali mzigo huu mzito ili wananchi wengi zaidi wasipate maambukizi haya,” amesema Rostam.
MFANYABIASHARA maarufu nchini Rostam Aziz (pichani kushoto) akiwa sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe.Paul Makonda wakipita kwenye mashine maalumu za kupuliza dawa ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Post a Comment