Featured

    Featured Posts

SERIKALI ZA KIGENI ZALAANI KUKAMATWA WANAHARAKATI WA DEMOKRASIA HONG KONG

  Serikali za kigeni zimekosoa kukamatwa kwa wanaharakati 15 wa Hong Kong wanaopigania demokrasia na ambao wanatuhumiwa kwa kupanga na kushiriki katika maandamano ya kuipinga serikali mwaka jana.
Miongoni mwa waliokamatwa ni wanasiasa wakongwe, tajiri wa vyombo vya habari na wanasheria waandamizi. Chama cha Kimataifa cha Wanasheria kimesema maafisa wa Hong Kong hawapaswi kukiuka haki za binaadamu na mfumo wa kisheria lazima uweke ulinzi dhidi ya ukiukaji wowote wa mamlaka wakati ulimwengu ukilishughulikia janga la virusi vya corona.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Marekani Mike Pompeo amesema China na wawakilishi wake mjini Hong Kong wanaendelea kuchukua hatua zisizoendana na ahadi zilizotolewa chini ya Tamko la Pamoja la China na Uingereza linalojumuisha uwazi, utawala wa sheria, na kuhakikisha kuwa Hong Kong inaendelea kufurahia kiwango cha juu cha uhuru.

Nchini Uingereza, Wizara ya Mambo ya Kigeni imesema serikali inatarajia ukamataji wowote na utaratibu wa mahakama vifanywe katika njia ya haki na uwazi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana