UBUNGO, Dar es Salaam
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Dar es Salaam, imefanya uzinduzu wa Kamati ya Maafa ya Wilaya katika hafla iliyofanyika leo, katika Ukumbi uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, na kufunguliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic.
Katika uzinduzi huo mwezeshaji alikuwa ni Mratibu wa timu ya Wataalam ya Maafa Mkoa wa Dar es Salaam Dk.Christopher Mnzava na Mratibu wa maafa Wilaya ya Ubungo Juliana Kibonde
Lengo/kazi ya kamati hiyo ni Kuhuisha masuala ya dharura na maafa katika mipango ya kimaendeleo, kufuatilia tishio la majanga na maafa wilayani na kuchukua hatua, kuainisha mahitaji na kutoa elimu, kufanya uchunguzi wa kutokea kwa maafa na uchoraji wa Ramani, kuunda timu ya ukabilianaji wa maafa na muundo wa kulinda jamii na kuhakikisha vifo vinavyotokana na dharula mbalimbali vinazuiliwa
Katika uzinduzi huo Mkurugenzi aliwaasa viongozi wa dini na asasi kuwa ni wajumbe ambao wataweza kufikisha taarifa ya mambo ambayo Manispaa inafanya na hata majanga mbalimbali yanapotokea watakuwa mawakala wazuri katika kuongelea hayo kwa wananchi.
"Kuna mambo mengi yanayotokea katika jamii kwa sasa, Kuna janga la korona nyie sasa ni watu ambao mtakuwa mstari wa mbele kuelimisha watu kwenye jamii zetu tuepukane na janga hili". Aliongeza Mkurugenzi.
Nae Dr. Nnzava alieleza kuwa ni nafasi ya kila mmoja kuhakikisha anatafuta mbinu na namna ambayo itatumika kudhibiti maafa na pia yanapotekea Maafa vifo hupungua endapo yakiratibiwa kiitalaam.
Mwisho Mratibu wa Maafa Manispaa ya Ubungo alishukuru kwa ujio wa wajumbe na kuomba kushirikiana bega kwa bega ili kusaidia Manispaa ya Ubungo katika suala zima la maafa.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
MANISPAA YA UBUNGO
Post a Comment