Featured

    Featured Posts

JAFO AUTAKA UONGOZI MPYA WA SHIRIKA LA ELIMU KUWA WABUNIFU



 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo (kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti mpya wa Shirika la Elimu Kibaha, Prof Rafael Chibunda (kulia) leo jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Robert Shillingi.
 Waziri wa Nchi Ofis ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara yake, pamoja na Viongozi wapya wa Shirika la Elimu Kibaha baada ya leo kuwakabidhi vitendea kazi.
 Mwenyekiti wa Shirika la Elimu Kibaha Mkoani Pwani, Prof Rafael Chibunda akizungumza baada ya kukabidhiwa vitendea kazi na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akizungumza na Viongozi na wajunbe wa Bodi ya Shirika la Eli
Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Elimu Kibaha Mkoani Pwani ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akitoa shukrani zake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo leo jijini Dodoma.

Charles James, Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo ameutaka Uongozi mpya wa Shirika la Elimu Kibaha Mkoani Pwani kuongeza ubunifu kwa kufanya miradi itakayokua na manufaa kwa shirika na Taifa kwa ujumla.

Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati alipokua akiwakabidhi vitendea kazi uongozi huo mpya chini ya Mwenyekiti wake, Prof Rafael Chibunda ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Cha Kilimo (SUA).

Shirika la Elimu Kibaha ni mojawapo ya Shirika kongwe nchini linalotoa huduma ya elimu na afya huku likisaidia mapambano dhidi ya maadui watatu ambao ni Maradhi, Ujinga na Umaskini.

Shirika hilo ambalo limetimiza miaka 50 toka kuanzishwa kwake ni chombo ambacho kimekua kikitoa elimu shuleni na inayohusu afya na kilimo na kutoa tiba na kinga kwa wananchi wanaozunguka maeneo jirani.

Akizungumza na Viongozi wa shirika hilo, Waziri Jafo amewataka kuendana na spidi ya Serikali ya Rais Magufuli katika kufanya kazi na kuleta matokeo chanya sambamba yatakayokua na manufaa kwa Taifa.

Amesema shirika hilo lazima liwe na athari chanya kwa wakazi wanaozunguka wilaya ya Kibaha na hiyo ndio kazi kubwa ambayo Bodi mpya inapaswa kufanya.

" Niwapongeze kwa kuteuliwa kuongoza shirika hili kongwe, mnapaswa kujua mmebeba maono ya Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na Rais Dk John Magufuli, nendeni mkafanye kazi kwa kutumia elimu zenu, uwezo wenu na uzoefu wenu. Kayaguseni maisha ya watanzania. Shirika linapaswa kujiendesha lenyewe kwa kuwa na rasimali zake.

Mmekua ni sehemu ya kutoa mafunzo kwenye sekta ya afya pia, pale kwenye Hospitali ya Tumbi mmetoa elimu na mafunzo kwa wataalam wetu, hili ni jambo kubwa mmefanya lakini mnapaswa kulifanya zaidi ya sasa," Amesema Jafo.

Ameutaka uongozi wa Shirika hilo kutumia ukubwa wa ardhi iliyopo wilayani Kibaha katika kufanya uwekezaji mkubwa ambao utakua na manufaa kwa shirika lao na kuipatia serikali pia mapato.

" Uwepo wa Shirika lenu pale Kibaha siyo faida kwa wakazi wa pale tu, inapaswa iwafikie hata watu wa pembezoni, mfano eneo jirani la Kiluvya pale hakuna Zahanati wala Kituo cha Afya, kwanini msiwajengee Zahanati ambayo itaokoa idadi kubwa ya watanzania wenzetu? Hapo mtakua mmeacha alama kwa watu wanaozunguka, " Amesema Jafo.

Amelitaka Shirika hilo kufanya uwezekaji mkubwa ikiwemo kujenga 'shopping mall' ya kisasa Kibaha ambayo italifanya shirika kuwa na nguvu kiuchumi lakini pia ikichangia pato la Taifa.


Amelipongeza shirika hilo kwa namna ambavyo limekua likitoa elimu ya ufundi kwa vijana wengi nchini wanaoenda kuchukua ujuzi kupitia Chuo chao cha FDC na kuwataka kuwafikia kundi kubwa la vijana zaidI.

" Kibaha ni mojawapo ya maeneo yenye ardhi kubwa, sasa chini ya Bodi hii mnapaswa kuitumia ardhi hii, mje na ubunifu wa kufanya uwekezaji utakaokua Tija kwa shirika.

Leo hii Kibaha inakua, mnapaswa mje na kitu kikubwa cha mfano, natamani nione Shopping Mall kubwa pale, angalieni uwekezaji utakaokua na tija kwa Taifa na shirika, hii itawafanya watu wapende uwepo wenu hapo," Amesema Waziri Jafo.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Shirika hilo, Prof Rafael Chibunda amemshukuru Rais Dk John Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuongoza shirika hilo kongwe nchini huku akiahidi kutumia elimu na uzoefu wake ili shirika hilo liwe msaada kwa serikali katika mapambano dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi.

Amesema kwenye Bodi hii mpya hakutakua na mjumbe ambaye hatokua na mchango kwenye kikao na kwamba hawatohitaji wajumbe ambao watakua wakija kwenye kikao kuchat au kuwa bize na mitandao ya kijamii.

"Shukrani kwa Rais Magufuli kwa kuniamini kusimamia shirika hili kubwa lenye msaada mkubwa kwa Taifa hili kwenye sekta ya elimu na afya, hii ni imani kubwa na hakika sitomuangusha Rais ambaye ameniamini," Amesema Prof Chibunda.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana