Featured

    Featured Posts

KABUGA, MSHUKIWA MKUU WA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA AKANUSHA TUHUMA DHIDI YAKE

Kabuga mwenye umri wa miaka 84 jana Jumatano kupitia mkalimani aliimbia Mahakama ya Ufaransa kuwa, "yote haya ni urongo, sijaua Watutsi wowote, nilikuwa nafanya kazi nao."
Mshukiwa huyo anaandamwa na makosa saba yakiwemo ya uchochezi wa mauaji ya kimbari, jinai dhidi ya binadamu na kuunda na kufadhili kundi la wanamgambo wa kikabila ambalo lilitekeleza mauaji hayo ya kimbari ya 94.
Hapo jana pia, mahakama hiyo ya Ufaransa ilikataa kumuachia huru Kabuga. Mawakili wake walikuwa wameiomba mahakama hiyo imuachie huru kwa dhamana kutokana na hali yake mbaya ya kiafya na imuwekea chini ya uangalizi wa korti. 
Mtuhumiwa huyo mkuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda alikamatwa na polisi mjini Paris mapema mwezi huu, baada ya kuukwepa mkono wa sheria kwa zaidi ya miaka 26.
Felicien Kabuga mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda
Kabuga alikuwa miongoni mwa watuhumiwa 11 waliokuwa wakisakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) na hata kutangazwa dau la dola milioni tano kwa atakayetoa taarifa za kutiwa mbaroni mshukiwa huyo.
Mauaji ya kimbari ya Rwanda yalijiri kwa muda wa siku 100 kuanzia Aprili 6 mwaka 1994 baada ya Rais Juvanal Habyarimana na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira, wote Wahutu, kupoteza maisha wakati ndege yao ilipotunguliwa katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali. Karibu watu milioni moja waliuawa katika mauaji hayo ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana