Waandamanaji wakusanyika nje ya Ikulu pamoja na maeneo mengine juu ya kifo cha raia mweusi George Floyd.
Waandamanaji wanakabiliana na polisi katika miji mbalimbali nchini Marekani juu ya mauaji ya raia mweusi wa Marekani ambaye hakuwa na silaha aliyekufa mikononi mwa polisi huko Minneapolis.
Gavana wa Minnesota amesema kwamba kifo cha George Floyd aliyekuwa kizuizini kimeonesha mauaji ya kiholela.
New York, Atlanta na maeneo mengine yamekuwa yakishuhudia ghasia huku Ikulu ya Marekani ikiwekewa katika hatua ya kusalia ndani kwa muda mfupi.
Aliyekuwa afisa wa polisi katika eneo la Minneapolis ameshtakiwa kwa mauaji kutokana na kifo hicho.
Hali ilivyo hadi kufikia sasa?
Ijumaa jioni, Ikulu ya Marekani ilikuwa inatekeleza hatua ya kusalia ndani baaada ya maandamano kufanyika nje ya Ikulu hiyo. "Siwezi kupumua," waandamanji walikuwa wanapaza sauti na kusema maneno hayo, wakiigizia maneno ya mwisho ya Bwana Floyd.
Kifo hicho kinafuatia vile vya Michael Brown, Eric Garner, mwanaume mweusi aliyekufa baada ya kukamatwa na polisi mjini New York, 2014 na wengine wengi tangu kuanza kwa vuguvugu 'Black Lives Matter' yaani 'Maisha ya mtu mweusi
Wakati huohuo, bado hatua ya kutotoka nje usiku inatekelezwa kwa miji ya Minneapolis-Saint Paul, kuanzia 20:00 usiku hadi 06:00 asubuhi Ijumaa na Jumamosi jioni.
Alhamisi, wakati wa maandano ya usiku wa tatu kwasababu ya kifo cha Bwana Floyd, kituo cha polisi kilichomwa moto. Majengo kadhaa yamechomwa moto vilevile, na siku za hivi karibuni wamekuwa wakichoma na kuhabu mali za watu.
Ijumaa katika mji wa Atlanta, gari la polisi pia lilichomwa moto wakati ambapo waandamanji walikuwa wamekusanyika karibu na ofisi za shirika la utangazaji la CNN.
Maandamano hayo pia yameshuhudiwa kwengineko, ikiwemo miji ya New York, Los Angeles, Chicago, Denver, Houston, Louisville, Phoenix, Columbus na Memphis.
Tayari raia walikuwa na hasira juu ya kuuawa kwa raia wengine wawili weusi, Ahmaud Arbery mji wa Georgia na Breonna Taylor.
Waandamanaji walikiuka hatua ya kusalia ndani Ijumaa huku wengine wakichoma moto magari katika maeneo ambayo zimamoto ilishindwa kufika.
Televisheni pia zimeonesha watu wakiharibu mali katika eneo la Minneapolis na idadi ya maafisa wa polisi waliofika kurejesha hali kuwa ya kawaida ikiwa ndogo.
Hadi kufikia karibu saa sita usiku hapo ndipo polisi walipoonekana katika maeneo mengine kwa mujibu wa gazeti la the Minneapolis Star Tribune.
Gavana wa jimbo Tim Walz, katika mkutano na wanahabari, ameelezea hali ilivyo kuwa mbaya, hatari na ambayo haijawahi kushuhudiwa hapo kabla.
Alisema kwamba maafisa waliopelekwa kurejesha amani idadi yao ndio kubwa zaidi katika historia lakini waandamanaji ni wengi kuwaliko. Ameongeza kuwa waliojitokeza hawajali tena kuhusu hatua ya kusalia ndani.
Jeshi pia limewekwa katika tahadhari ya uwezekano wa wao kupelekwa eneo la Minneapolis kama hatua ya kurejesha amani.
Katika mji wa New York, eneo la Brooklyn, waandamanaji walikabiliana na polisi kwa kuwarushia chochote walichoona, kuwasha moto na kuchoma moto magari ya polisi.
Maafisa kadhaa wa polisi walijeruhiwa.
Mayor Bill de Blasio aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter: "Hatutaki kushuhudia usiku mwengine kama huu."
Tayari raia walikuwa na hasira juu ya kuuawa kwa raia wengine wawili weusi, Ahmaud Arbery mji wa Georgia na Breonna Taylor.
Polisi anayehusishwa na mauaji ya George Floyd ameshtakiwa
Aliyekuwa afisa wa Minneapolis amekamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya mauaji baada ya kutokea kwa kifo cha mwanamume mweusi ambaye hakuwa na silaha aliyekuwa kizuizini.
Derek Chauvin, ambaye ni mzungu, alioneshwa kwenye video akipiga magoti juu ya shingo ya George Floyd mwenye umri wa miaka 46, Jumatatu. Yeye pamoja na maafisa wengine watatu wamekamatwa.
Maandamano ya siku kadhaa katika mji wa Minnesota yamesababisha uharibufu wa mali na kuchoma moto majumba ambayo pia yamesambaa katika maeneo mengine nchini Marekani.
Tukio hilo limesababisha hasira na ghadhabu nchini humo juu ya matukio mengine kama hayo ambapo polisi huwaua raia weusi wasiokuwa na hatia.
Mwendesha mashtaka alisema nini?
Mwendesha mashtaka Mike Freeman wa kaunti ya Hennepin alisema Bwana Chauvin alishtakiwa kwa makosa ya mauaji kiwango cha tatu huku kiwango cha pili kikiwa ni kuua bila kukusudia,
Aliongeza kuwa anatarajia kwamba wale maafisa wengine watatu pia nao watafunguliwa mashtaka lakini hakutoa maelezo zaidi.
Bwana Freeman alisema kuwa ofisi yake itaendesha kesi hii mara moja punde tu baada ya wao kupokea ushahidi".
"Hatujawahi kufungua mashtaka kwa haraka kiasi hiki dhidi ya afisa wa polisi," alisema.
Kwa mujibu wa aliye mshitaki kwa makosa ya uhalifu, Bwana Chauvin alichukua hatua akiwa na nia ya kushambulia bila kuzingatia ubinadamu.
George Floyd alikufa vipi?
Ripoti kamili ya madaktari bado haijatolewa lakini malalamishi yanasema kwamba upasuaji uliofanywa kama sehemu ya uchunguzi baada ya kifo cha Bwana Floyd, haukupata ushahidi wowote wa shinikizo la kubanwa kifua au kunyongwa.
Matokeo ya uchunguzi wa daktari yameonesha kwamba Bwana Floyd alikuwa na matatizo ya moyo na mchanganyiko wa yote hayo mawili, pengine vichocheo fulani katika mfumo wake na kukandamizwa na maafisa huenda kulichangia kifo chake.
Ripoti inasema kwamba Bwana Bwana Chauvin aliweka goti lake juu ya shingo ya Bwana Floyd na kumkandamiza kwa dakika 8 na sekunde 46 - karibia dakika tatu ambapo Bwana Bwana Floyd hakuamka tena.
Karibia dakika mbili kabla ya kuondoa goti lake maafisa wengine waliangalia kiganja cha mkono cha Bwana Floyd ikiwa bado mapigo ya moyo yapo lakini hawakuona chochote.
Alipelekwa katika Kituo cha Matibabu kaunti ya Hennepin kwa kutumia ambulansi na kusemekana kwamba amekufa karibia saa moja baadae.
Kitabu cha polisi huko Minnesota kinaonesha kwamba maafisa wa polisi walipata mafunzo ya kukandamiza shingo ya aliyekamatwa bila ya kuweka kushinikizo moja kwa moja kwenye njia ya kupumua na afisa anaweza kutumia goti lake chini ya sheria yake ya utumiaji wa nguvu.
Hii inachukuliwa kama njia ya kutumia nguvu bila kuua.
Trump alisema nini?
Akiwa katika Ikulu ya Marekani Ijumaa, Rais Donald Trump alitaja tukio hilo kama baya zaidi kutokea na kusema kwamba amezungumza na familia ya Bwana Floyd, aliyoieleza kama familia ya watu wazuri mno.
Alisema ametoa wito kwa idara ya haki kuharakisha uchunguzi iliyotangaza Ijumaa wa kutathmini ikiwa kuna ukiukaji wowote wa haki uliotekelezwa katika kifo cha Bwana Floyd.
Rais alisema pia wanaopora mali za watu hawastahili kuharibia wengine wengi ambao wanafanya maandamano yao kwa njia ya amani.
Awali alielezea wanaopora mali kama wahuni wanaokosea heshima kumbukumbu ya Bwana Floyd.
Aidha mtandao wa kijamii wa Twitter umemshtumu Bwana Trump kwa kusifia ghasia katika ujumbe wake alioandika: "Uporaji wa mali ukianza, ufyatuaji wa risasi unaanza."
Watu wamechukulia vipi tukio hili?
Familia ya Bwana Floyd na wakili wake, Benjamin Crump, ilisema kukamatwa kwa Floyd kunaruhusiwa lakini hilo limepitwa na wakati.
Familia hiyo ilisema inataka mshtakiwa ashtakiwe kwa makosa ya mauaji kiwango cha kwanza pamoja na kukamatwa kwa maafisa wengine waliokuwepo.
Taarifa hiyo pia inataka mji huo kubadilisha sera yake, ikisema: "Leo, familia ya George Floyd inalazimika kuelezea kwa watoto wake kwanini baba yao aliuawa na polisi kupitia video iliosambaa mtandaoni."
Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama pia nae alitoa maoni yake na kusema: "Hili halistahili kuwa jambo la kawaida kwa Marekani ya 2020."
Katika taarifa yake aliongeza: "Ikiwa tunataka watoto wetu kukua katika taifa lenye maadili ya juu, tunaweza na nilazime tuwe na maadili mema."
Gavana wa Minnesota Tim Walz alisema kukamatwa kwa afisa huyo wa polisi "ni ishara nzuri katika hatua ya kuhakikisha haki inatendeka".
Nini kilitokea wakati wa kukamatwa kwa Bwana Flyod?
Maafisa wa polisi walishuku kwamba Bwana Floyd alikuwa ametumia pesa bandia noti ya $20 (£16) na walikuwa wanajitahidi kumuingiza kwenye gari la polisi alipoanguka chini, akiwaambia kuwa yeye anatatizo la kuogopa anapowekwa kwenye sehemu yenye nafasi kidogo.
Kulingana na polisi, alikuwa amekataa maafisa hao wamkamate na hivyo kutiwa pingu.
Video hiyo haioneshi malumbano yalianza vipi lakini afisa wa polisi mzungu anaonekana akiwa amepiga goti juu ya shingo la Bwana Floyd huku akimkandamiza.
Bwana Floyd anaonekana akisema "tafadhali, nashindwa kupumua" na "usiniuwe".
Aliyekuwa mmiliki wa kilabu moja ya usiku amesema Bwana Chauvin na Bwana Floyd wote walikuwa wanafanyakazi kama walinzi wa kilabu yake kusini mwa Minneapolis hadi mwaka jana, ingawa haijabanika ikiwa wanajuana.Gavana wa Minnesota Tim Walz alisema kukamatwa kwa afisa huyo wa polisi "ni ishara nzuri katika hatua ya kuhakikisha haki inatendeka".
Nini kilitokea wakati wa kukamatwa kwa Bwana Flyod?
Maafisa wa polisi walishuku kwamba Bwana Floyd alikuwa ametumia pesa bandia noti ya $20 (£16) na walikuwa wanajitahidi kumuingiza kwenye gari la polisi alipoanguka chini, akiwaambia kuwa yeye anatatizo la kuogopa anapowekwa kwenye sehemu yenye nafasi kidogo.
Kulingana na polisi, alikuwa amekataa maafisa hao wamkamate na hivyo kutiwa pingu.
Video hiyo haioneshi malumbano yalianza vipi lakini afisa wa polisi mzungu anaonekana akiwa amepiga goti juu ya shingo la Bwana Floyd huku akimkandamiza.
Bwana Floyd anaonekana akisema "tafadhali, nashindwa kupumua" na "usiniuwe".
Aliyekuwa mmiliki wa kilabu moja ya usiku amesema Bwana Chauvin na Bwana Floyd wote walikuwa wanafanyakazi kama walinzi wa kilabu yake kusini mwa Minneapolis hadi mwaka jana, ingawa haijabanika ikiwa wanajuana.
Mtazamo: Maneno ambayo ni kitisho
Na Barrett Holmes Pitner
Kusema kuwa "uporoji ukianza, ufyatuaji risasi unaanza", Rais Donald Trump alirejelelea usemi wa Desemba 1967 kutoka kwa mkuu wa polisi wa Miami Walter Headley.
Alitumia maneno hayo kama tishio dhidi ya Wamerakani weusi huko Miami na kama sehemu ya sera yake ambapo alikuwa ameamua kutumia bunduki na mbwa kusitisha maandamano ya watetezi wa haki za kiraia.
Agosti 1968, wakati Richard Nixon anahutubia mkutano wa taifa wa chama cha Republican huko Miami, polisi wa eneo hilo waliuwaua waandamanaji watatu huku wengine 18 wakijeruhiwa na zaidi ya 200 walikamatwa.
Ghasia sawa na hizo ambapo maafisa wa polisi wanashambulia raia zilijitokeza miaka ya 1960 wakati raia weusi wa Marekani walikuwa wanapigania haki yao ya kiraia na kupiga kura.
Post a Comment